Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Timotheo 2:14 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

14 Uwakumbushe bayo, ukiwaonya katika Bwana, wasiwe na mashindano ya maneno, yasiyo na faida, bali huwaharibu wasikiao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Basi, wakumbushe watu wako mambo haya na kuwaonya mbele ya Mungu waache ubishi juu ya maneno. Ubishi huo haufai, ila huleta tu uharibifu mkuu kwa wale wanaousikia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Basi, wakumbushe watu wako mambo haya na kuwaonya mbele ya Mungu waache ubishi juu ya maneno. Ubishi huo haufai, ila huleta tu uharibifu mkuu kwa wale wanaousikia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Basi, wakumbushe watu wako mambo haya na kuwaonya mbele ya Mungu waache ubishi juu ya maneno. Ubishi huo haufai, ila huleta tu uharibifu mkuu kwa wale wanaousikia.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Endelea kuwakumbusha mambo haya, ukiwaonya mbele za Mungu waache kushindana kwa maneno ambayo hayana faida yoyote, bali huwaangamiza tu wale wanaoyasikia.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Endelea kuwakumbusha mambo haya ukiwaonya mbele za Bwana Isa waache kushindana kwa maneno ambayo hayana faida yoyote bali huwaangamiza tu wale wanaoyasikia.

Tazama sura Nakili




2 Timotheo 2:14
30 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana atafaidiwa mtu nini akiupata ulimwengu wote, na kupata khasara ya roho yake? au mtu atatoa nini badala ya roho yake?


Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa shetani, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyoka?


Kwa kuwa tumesikia ya kwamba watu waliotoka kwetu wamewasumbueni kwa maneno yao, wakipotosha roho zenu, wakisema, ya kuwa hamna buddi kutahiriwa na kuishika Torati, ambao sisi hatukuwapa agizo lo lote;


LAKINI yeye aliye dhaifu wa imani, mkaribisheni, illakini msimhukumu mawazo yake.


mkageukia injili ya namna nyingine; wala si nyingine. Lakini wapo watu wawataabishao na watakao kuigeuza injili ya Kristo.


Bassi nasema neno bili, tena nashuhudu katika Bwana, tangu sasa msienende kama Mataifa waendavyo, katika ubatili wa nia zao,


ILIYOBAKI, ndugu, tunakusihini na kukuonyeni kuenenda katika Bwana Yesu, kama mlivyopokea kwetu, jinsi iwapasavyo kuenenda na kumpendeza Mungu, kama na muavyoenenda, mpate kuzidizidi sana.


Twawaagizeni, ndugu, katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo, jitengeni nafsi zenu na killa ndugu aendae bila utaratibu, wala si kwa kufuata mapokeo mliyoyapokea kwetu.


wala wasiangalie hadithi na nasaba zisizo na ukomo, ziletazo maswali wala si ujenzi wa Mungu ulio katika imani; bassi sasa nakuagiza vivyo hivyo.


wengine wakikosa bayo wamepotea, wakigeukia maneno ya ubatili;


Jitahidi kupata utawa. Maana, kujitahidi kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo, hali utawa hufaa kwa mambo yote; maana nna ahadi ya uzima wa sasa na wa ule utakaokuwa.


Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Bwana Kristo Yesu, na mbele ya malaika wateule, yatende hayo pasipo kuhukumu kwa haraka; usifanye neno lo lote kwa upendeleo.


Nakuagiza mbele za Mungu avipae vitu vyote uzima, na mbele za Kristo Yesu aliyeungama maungamo yale mazuri mbele ya Pontio Pilato,


Kwa sababu hiyo nakukumbusha, uichochee karama ya Mungu iliyo ndani yako kwa kuwekewa mikono yangu.


Jiepushe na maneno yasiyo na maana, yasiyo ya dini; maana wataendelea zaidi katika maovu;


Walakini yakatae maswali ya upumbavu, yasiyo na elimu, ukijua ya kuwa huzaa magomvi:


NAKUSHUHUDIA mbele za Mungu, na Bwana Yesu Kristo, atakaewahukumu walio hayi na waliokufa, kwa kudhihiri kwake, na kwa ufalme wake;


WAKUMBUSHE kujinyenyekea kwa wenye uwezo na mamlaka, na kutii, na kuwa tayari kwa killa kazi njema,


Msichukuliwe na mafundisho ya namna nyingine nyingine, na ya kigeni; maana ni vizuri moyo ufanywe imara kwa neema, wala si kwa vyakula, ambavyo wao waliokwenda navyo bawakupata faida.


Nami naona ni haki, maadam nipo mimi katika maskani hii, kuwaamsheni kwa kuwakumhusheni.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo