Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Timotheo 2:12 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

12 kama tukistahimili, tutamiliki pamoja nae pia; kama tukimkana yeye, yeye nae atatukana sisi:

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Tukiendelea kuvumilia, tutatawala pia pamoja naye. Tukimkana, naye pia atatukana.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Tukiendelea kuvumilia, tutatawala pia pamoja naye. Tukimkana, naye pia atatukana.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Tukiendelea kuvumilia, tutatawala pia pamoja naye. Tukimkana, naye pia atatukana.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Kama tukistahimili, pia tutatawala pamoja naye. Kama tukimkana, naye atatukana.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Kama tukistahimili, pia tutatawala pamoja naye. Kama tukimkana yeye, naye atatukana sisi.

Tazama sura Nakili




2 Timotheo 2:12
29 Marejeleo ya Msalaba  

Bali mtu ye yote atakaenikana mbele ya watu, nami nitamkana mbele ya Baba yangu aliye mbinguni.


Petro akamwambia, Ijaponipasa kufa nawe, sitakukana. Na wanafuuzi wote wakasema vivi hivi.


Petro akalikumbuka lile neno la Yesu aliloambiwa nae, Kabla ya kuwika jogoo, utanikana marra tatu. Akatoka nje, akalia kwa majonzi.


Angalieni, tunapanda kwenda Yerusalemi: na Mwana wa Adamu atatiwa mikononi mwa makuhani wakuu na waandishi,


Maana killa mtu atakaenionea haya mimi, na maneno yangu, katika kizazi hiki cha zina na dhambi, Mwana wa Adamu atamwonea haya yeye atakapokuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu.


Nae aliyenikana mbele ya watu, atakanwa mbele za malaika wa Mungu.


Nanyi ndinyi mliodumu pamoja nami katika majaribu yangu. Nami nawawekea ninyi ufalme, kama alivyoniwekea Baba yangu;


mpate kula na kunywa mezani pangu katika ufalme wangu, na kuketi katika viti vya enzi, mkiwahukumu kabila thenashara za Israeli.


Kwa sababu killa mtu atakaenionea haya mimi na maneno yangu, Mwana wa Adamu atamwonea haya huyo atakapokuja katika utukufu wake, na wa Baba yake, na wa malaika watakatifu.


wakifanya imara roho za wanafunzi na kuwaonya wakae katika imani, na ya kwamba imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya shidda nyingi.


Kwa maana ikiwa kwa kuteleza mtu mmoja mauti ilitawala kwa sababu ya yule mmoja, zaidi sana wao wapokeao wingi wa neema, na kile kipawa cha haki, watatawala katika uzima kwa yule mmoja, Yesu Kristo.


kama tu watoto, bassi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja nae illi tutukuzwe pamoja nae.


wala hamwogopi adui zenu, katika neno lo lote; kwao hao ni ishara wazi ya kupotea, bali kwenu ninyi ni ishara ya wokofu, nao wa Mungu.


Lakini mtu asiyewatunza walio wake na khassa watu wa nyumba yake ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko yeye asiyeamini.


Kwa maana kuna watu wamejiingiza kwa siri, watu walioandikiwa zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufasiki, nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na Bwana wetu Yesu Kristo.


na kutufanya kuwa ufalme, na makuhani kwa Mungu, Baba yake: utukufu na ukuu una Yeye hatta milele na milele. Amin.


Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na uvumilivu wa Yesu Kristo, nalikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, kwa ajili ya Neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu.


Napajua ukaapo, ndipo penye kiti cha Shetani: nawe walishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hatta katika siku za Antipa shahidi wangu mwaminifu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani.


Nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, wakapewa hukumu: nikaona roho zao waliokatwa kichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia nyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea alama yake katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; wakawa hayi, wakamiliki pamoja na Kristo miaka elfu.


Yu kheri, mtakatifu, aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina nguvu; bali watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao watamiliki pamoja nae miaka elfu.


Kwa kuwa ulilishika neno la uvumilivu wangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kujaribiwa iliyo tayari kuujia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya inchi.


Yeye asbindae, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda, nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.


Najua matendo yako. Tazama, nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako, wala hapana awezae kuufunga, kwa kuwa unazo nguvu kidogo, nawe ulilitunza neno langu, wala hukulikana jina langu.


ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa killa kabila na lugha na jamaa na taifa, ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu: nao wanamiliki juu ya inchi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo