Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Timotheo 1:5 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

5 nikikumbuka imani uliyo nayo isiyo na unafiki, iliyokaa kwanza katika bibi yako Loi, na katika mama yako Euniki; aa ninasadiki ya kwamba na wewe nawe unayo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Naikumbuka imani yako ya kweli, imani aliyokuwa nayo nyanya yako Loisi, na pia mama yako Eunike. Nina hakika kwamba wewe pia unayo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Naikumbuka imani yako ya kweli, imani aliyokuwa nayo nyanya yako Loisi, na pia mama yako Eunike. Nina hakika kwamba wewe pia unayo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Naikumbuka imani yako ya kweli, imani aliyokuwa nayo nyanya yako Loisi, na pia mama yako Eunike. Nina hakika kwamba wewe pia unayo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Nimekuwa nikiikumbuka imani yako ya kweli, waliokuwa nayo bibi yako Loisi na mama yako Eunike, na ninasadiki sasa wewe pia unayo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Nimekuwa nikiikumbuka imani yako ya kweli, waliokuwa nayo bibi yako Loisi na mama yako Eunike na ambayo mimi ninasadiki sasa wewe pia unayo.

Tazama sura Nakili




2 Timotheo 1:5
25 Marejeleo ya Msalaba  

Yesu akamwona Nathanaeli akija kwake, akamtaja khabari zake, Tazama, huyu ni Mwisraeli kweli kweli, hamna hila ndani yake.


AKAFIKA Derbe na Lustra, na hapo palikuwa na mwanafunzi mmoja jina lake Timotheo, mwana wa mwanamke mmoja Myahudi aliyeamini: lakini baba yake alikuwa Myunani.


Kwa maana mfalme anajua khabari za mambo haya, na naweza kusema nae bila khofu, kwa sababu najua sana ya kuwa hapana neno moja katika hayo asilolijua; kwa maana jambo hilo halikutendeka pembeni.


Najua, tena nimehakikishwa sana katika Bwana Yesu, ya kuwa hakuna kitu kilicho najis asili yake, lakini kwake huyu akionae kitu kuwa najis, kwake huyo kitu kile ni najis.


Mtu mmoja afanya tofauti kati ya siku na siku; mwingine aona siku zote kuwa sawa sawa. Killa mtu athuhutike katika akili zake mwenyewe.


Na mimi mwenyewe, ndugu zangu, nimehakikishwa kwa khahari zenu kama ninyi nanyi mmejaa wema, mmejazwa elimu yote, tena mwaweza kuonyana.


akijua hakika ya kuwa Mungu aweza kufanya yale aliyoahidi.


Kwa maana tumekwisha kujua hakika ya kuwa hatta mauti haiwezi kututenga, wala nzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala wenye uwezo, wala yaliyopo, wala yatakayokuwa,


katika kuwa safi, katika elimu, katika uvumilivu, katika utu wema, katika Roho Mtakatifu, katika upendo usio unafiki,


Bali kusudi la mausia hayo ni upendo utokao katika moyo safi na dhamiri njema, na imani isiyo na unafiki:


Ukiwakumhusha ndugu hayo, utakuwa mkhudumu mwema wa Yesu Kristo, na mzoevu wa maneno ya imani, na ya mafundisho yale mazuri uliyoyafuata.


Kwa sababu hiyo nimepata mateso haya, wala sitahayariki: maana namjua yeye niliyemwamini, na kusadiki kwamba aweza kukilinda kile nilichakiweka amana kwake hatta siku ile.


na ya kuwa tangu utoto umeyajua maandiko matakatifu, yawezayo kukuhekimisha hatta upate wokofu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu.


Hawa wote wakafa katika imani, wasizipokee zile ahadi, bali wakiziona tokea mbali na kuzisalimu, na kukiri kwamba walikuwa wageni, na wasafiri juu ya inchi.


Lakini, wapenzi, ijapokuwa twanena hayo, katika khabari zenu tumesadiki mambo yaliyo mazuri zaidi, na yaliyo na wokofu:


Mkiisha kujisafisha roho zenu kwa kuitii kweli, kwa Roho, kiasi cha kuufikilia upendano usio na unafiki, bassi jitahidini kupendana kwa moyo;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo