Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Timotheo 1:1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 PAOLO, mtume wa Yesu Kristo, kama alivyopenda Mungu, kwa ahadi ya uzima ulio katika Yesu Kristo:

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Mimi Paulo, ambaye Mungu alitaka niwe mtume wa Kristo Yesu ili niutangaze ule uhai tulioahidiwa katika kuungana na Kristo Yesu,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Mimi Paulo, ambaye Mungu alitaka niwe mtume wa Kristo Yesu ili niutangaze ule uhai tulioahidiwa katika kuungana na Kristo Yesu,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Mimi Paulo, ambaye Mungu alitaka niwe mtume wa Kristo Yesu ili niutangaze ule uhai tulioahidiwa katika kuungana na Kristo Yesu,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Paulo mtume wa Al-Masihi Isa kwa mapenzi ya Mungu, kulingana na ile ahadi ya uzima ulio ndani ya Al-Masihi Isa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Paulo mtume wa Al-Masihi Isa kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu, kulingana na ile ahadi ya uzima uliomo ndani ya Al-Masihi Isa.

Tazama sura Nakili




2 Timotheo 1:1
29 Marejeleo ya Msalaba  

nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe, wala hakuna mtu atakaewapokonya katika mkono wangu.


Na uzima wa milele ni huu, wakujue wewe, Mungu wa peke yake, wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.


Amin, amin, nawaambieni, Alisikiae neno langu na kumwamini yeye aliyenipeleka ana uzima wa milele, wala hafiki hukumuni, bali amepita toka mauti hatta uzima.


Na mapenzi yake aliyenipeleka ni haya ya kwamba killa amtazamae Mwana na kumwamini awe ua uzima wa milele, nami nitamfufua siku ya mwisho.


Ailae nyama yangu na kuinywa damu yangu ana uzima wa milele; mimi nitamfufua siku ya mwisho.


PAOLO, mtumwa wa Yesu Kristo, aliyeitwa kuwa mtume, na kuwekwa aikhubiri Injili ya Mungu,


illi, kama vile dhambi ilivyotawaia katika mauti, vivyo hivyo kwa njia ya haki neema itawale hatta uzima wa milele kwa Yesu Kristo Bwana wetu.


Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; hali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.


PAOLO, aliyeitwa kuwa mtume wa Yesu Kristo kwa mapenzi ya Mungu, na Sosthene ndugu yetu,


PAOLO, mtume wa Yesu Kristo kwa mapenzi ya Mungu, na Timothieo ndugu yetu, kwa kanisa la Mungu lililo katika Korintho, pamoja na watakatifu wote walio katika inchi yote ya Akaia:


Maana ahadi zote za Mungu zilizopo katika yeye ni ndiyo; na katika yeye ni Amin, Mungu apate kutukuzwa kwa kazi yetu.


Maana ninyi nyote ni wana wa Mungu kwa njia ya imani katika Yesu Kristo.


Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote ni mmoja katika Kristo Yesu.


ya kwamba mataifa ni warithi pamoja nasi wa urithi mmoja, na wa mwili mmoja, na washiriki pamoja nasi ahadi yake iliyo katika Kristo kwa njia ya injili;


wakijiwekea akiba iwe msingi mzuri kwa wakati ujao illi wapate uzima wa milele.


na sasa inadhihirishwa kwa kufunuliwa kwake Mwokozi wetu Yesu Kristo, aliyebatili mauti na kuufunua uzima ua kutoa kuharibika, kwa ile Injili,


Shika sura ya maneno yenye uzima uliyoyasikia kwangu, katika imani na upendo uiio katika Kristo Yesu.


aliyetuokoa akatuita kwa wito mtakatifu, si kwa kadiri ya matendo yetu, bali kwa kadiri ya makusudi yake mwenyewe na neema yake, tuliyopewa sisi katika Kristo Yesu, kabla ya nyakati za zamani;


BASSI wewe, mwanangu, uwe hodari katika neema iliyo katika Kristo Yesu.


Kwa ajili ya hilo nastahimili yote, kwa ajili ya wateule, wao nao waupate wokofu ulio katika Kristo Yesu pamoja ua utukufu wa milele.


Ushiriki taabu pamoja nami, kama askari mwema wa Yesu Kristo.


na ya kuwa tangu utoto umeyajua maandiko matakatifu, yawezayo kukuhekimisha hatta upate wokofu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu.


katika tumaini la nzima wa milele, ambao Mungu asiyeweza kusema nwongo aliuahidi kabla ya nyakati za zamani;


kwa Tito, mwanangu katika imani tuishirikiyo: Neema na rehema na amani zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Bwana Yesu Kristo, Mwokozi wetu.


Na kwa sababu hii yu mjumbe wa agauo jipya, illi, mauti ikiisha kufanyika kwa kukomboa makosa ya katika agano la kwanza, walioitiwa waipokee ahadi ya urithi wa milele.


Na hii ndiyo ahadi alivyowaahidia ninyi, uzima wa milele.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo