Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Petro 3:17 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

17 Bassi, wapenzi, mkitangulla kujua haya, jilindeni nafsi zenu, msije mkachukuliwa na kosa la hawo wakhalifu, mkaanguka na kuuacha uthubutifu wenu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Lakini nyinyi, wapenzi wangu, mmekwisha jua jambo hili. Basi, muwe na tahadhari msije mkapotoshwa na makosa ya waasi, mkaanguka kutoka katika msimamo wenu imara.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Lakini nyinyi, wapenzi wangu, mmekwisha jua jambo hili. Basi, muwe na tahadhari msije mkapotoshwa na makosa ya waasi, mkaanguka kutoka katika msimamo wenu imara.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Lakini nyinyi, wapenzi wangu, mmekwisha jua jambo hili. Basi, muwe na tahadhari msije mkapotoshwa na makosa ya waasi, mkaanguka kutoka katika msimamo wenu imara.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Basi, ninyi wapendwa, kwa kuwa mmekwisha kujua mambo haya, jilindeni msije mkachukuliwa na kosa la watu hao waasi na kuanguka kutoka kwa uthabiti wenu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Basi, ninyi wapenzi, kwa kuwa mmekwisha kujua mambo haya, jilindeni msije mkachukuliwa na kosa la watu hao waasi na kuanguka kutoka kwenye uthabiti wenu.

Tazama sura Nakili




2 Petro 3:17
26 Marejeleo ya Msalaba  

Imekuwaje hamkufahamu ya kuwa si kwa sababu ya mkate naliwaambieni, jihadharini na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo?


Yesu akawaambia, Angalieni, jihadharini na chachu ya Mafarisayo na Masudukayo.


Jihadharini na manabii wa uwongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa wa mwitu wakali.


Lakini nimewaambieni haya, illi kusudi saa ile itakapokuja myakumbuke ya kuwa mimi naliwaambieni. Haya sikuwaambieni tangu mwanzo, kwa sababu nalikuwa pamoja nanyi.


Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali.


Kwa sababu bao ndio wasiomtumikia Bwana wetu Kristo, bali matumbo yao wenyewe; na kwa maneno laini na ya kujipendekeza waidanganya mioyo ya watu wasio wabaya.


Bassi anaejidhani amesimama aangalie asianguke.


Bassi, ndugu wapendwa, mwe imara, msiotikisika, mkizidi sana kutenda kazi ya Bwana siku zote, kwa kuwa taabu yenu siyo burre katika Bwana.


Lakini naogopa; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikara zenu, mkauacha unyofu wenu kwa Kristo.


Mmetengwa na Kristo, ninyi mtakao kufanyiziwa wema kwa sharia; mmeanguka toka hali ya neema.


illi tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukulivva kwa killa upepo wa elimu, kwa bila ya watu, kwa ujanja, tukifuata njia za udanganyifu;


Jihadharini na mbwa, jihadharini nao watendao mabaya, jihadharini nao wajikatao.


Maana nijapokuwa sipo kwa mwili, illakini nipo pamoja nanyi kwa roho, nikifurahi na kuuona utaratibu wenu na uthabiti wa imani yenu katika Kristo.


Angalieni intu asiwateke kwa filosofia yake na madanganya matupu, kwa jinsi ya mapokeo ya wana Adamu, kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu, wala si kwa jinsi ya Kristo.


Nawe ujibadhari na huyo, kwa sababu aliyapinga sana maneno yetu.


Kwa maana tumekuwa washirika wa Kristo, kama tukishikamana na mwanzo wa uthabiti wetu mpaka mwisho;


mpingeni, mkiwa imara katika imani, mkijua ya kuwa mateso yaleyale yanatimizwa kwa ndugu zenu walioko duniani.


akamwokoa Lut, aliyehuzunishwa na mwenendo wa uasharati wa hawo wakhalifu;


WAPENZI, waraka huu ndio wa pili niwaandikiao ninyi; katika hizo naziamsha nia zenu sali kwa kuwakumbusheni,


Bassi, kumbuka ulikoanguka, nkatubu, ukayatende matendo ya kwanza. Lakini, usipotenda hivyo, naja kwako upesi, nitaondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo