Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Petro 3:1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 WAPENZI, waraka huu ndio wa pili niwaandikiao ninyi; katika hizo naziamsha nia zenu sali kwa kuwakumbusheni,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Wapenzi wangu, hii ni barua ya pili ninayowaandikia. Katika barua hizo mbili nimejaribu kufufua fikira safi akilini mwenu kwa kuwakumbusheni mambo haya.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Wapenzi wangu, hii ni barua ya pili ninayowaandikia. Katika barua hizo mbili nimejaribu kufufua fikira safi akilini mwenu kwa kuwakumbusheni mambo haya.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Wapenzi wangu, hii ni barua ya pili ninayowaandikia. Katika barua hizo mbili nimejaribu kufufua fikira safi akilini mwenu kwa kuwakumbusheni mambo haya.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Wapendwa, huu ndio waraka wangu wa pili ninaowaandikia. Katika nyaraka hizi mbili ninajaribu kuziamsha nia zenu safi kwa mawazo makamilifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Wapenzi, huu ndio waraka wangu wa pili ninaowaandikia. Katika nyaraka hizi mbili ninajaribu kuziamsha nia zenu safi kwa mawazo makamilifu.

Tazama sura Nakili




2 Petro 3:1
15 Marejeleo ya Msalaba  

Wa kheri walio na moyo safi; maana hawo watamwona Mungu.


Nimetangulia kuwaambia: na kama vile nilipokuwapo marra ya pili, vivyo hivyo sasa nisipokuwapo natangulia kuwaambia wao waliofanya dhambi zamani, na wengine wote, ya kwamba, nikija, sitahurumia:


Usimwekee mtu mikono kwa haraka, wala usishiriki dhambi za watu wengine.


Kwa sababu hiyo nakukumbusha, uichochee karama ya Mungu iliyo ndani yako kwa kuwekewa mikono yangu.


Lakini, wapenzi, ijapokuwa twanena hayo, katika khabari zenu tumesadiki mambo yaliyo mazuri zaidi, na yaliyo na wokofu:


Mkiisha kujisafisha roho zenu kwa kuitii kweli, kwa Roho, kiasi cha kuufikilia upendano usio na unafiki, bassi jitahidini kupendana kwa moyo;


Mapenzi, nakusihini kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho;


Kwa hiyo, wapenzi, kwa kuwa mnatazamia hayo, fanyeni bidii illi muonekane kuwa hamna mawaa au aibu mbele yake, katika amani.


Bassi, wapenzi, mkitangulla kujua haya, jilindeni nafsi zenu, msije mkachukuliwa na kosa la hawo wakhalifu, mkaanguka na kuuacha uthubutifu wenu.


Lakini, wapenzi, msilisahau neno hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu kama siku moja.


Tena napenda kuwakumbusha, ijapo mmekwisha kujua haya yote, ya kwamba Bwana, baada ya kuwaokoa watu katika inchi ya Misri, aliwaharibu wasioamini.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo