Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Petro 2:4 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

4 Kwa maana kama vile Mungu hakuwaachilia malaika waliokosa, bali aliwatupa shimoni, akawatia katika mafungo ya giza, walindwe hatta ije hukumu;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Malaika walipotenda dhambi, Mungu hakuwahurumia, bali aliwatupa katika moto wa Jehanamu ambako wamefungwa wakingojea siku ile ya hukumu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Malaika walipotenda dhambi, Mungu hakuwahurumia, bali aliwatupa katika moto wa Jehanamu ambako wamefungwa wakingojea siku ile ya hukumu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Malaika walipotenda dhambi, Mungu hakuwahurumia, bali aliwatupa katika moto wa Jehanamu ambako wamefungwa wakingojea siku ile ya hukumu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Kwa maana, kama Mungu hakuwasamehe malaika walipotenda dhambi, bali aliwatupa Kuzimu katika vifungo vya giza wakae humo hadi ije hukumu;

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Kwa maana, kama Mwenyezi Mungu hakuwasamehe malaika walipotenda dhambi, bali aliwatupa kuzimu katika vifungo vya giza wakae humo mpaka ije hukumu;

Tazama sura Nakili




2 Petro 2:4
25 Marejeleo ya Msalaba  

Kisha atawaambia na wale walio mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, kwenda katika moto wa milele, aliowekewa tayari Shetani na malaika zake:


Wakapiga kelele, wakinena, Tuna nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu? Je, umekuja kutuadhibu kabla ya muhulla?


akalia kwa sauti kuu akanena, Nina nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye juu? Nakusihi, uniapie kwa Mungu kwamba hutaniadhibu.


Akawaambia, Nalimwona Shetani kama umeme akianguka toka mbinguni.


Akamsihi asiwaamuru waende zao hatta abusso.


Ninyi wa baba yenu Shetani, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzifanya. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo, wala hakusimama katika kweli kwa kuwa kweli hamna ndani yake. Asemapo uwongo, husema yaliyo yake mwenyewe, kwa sababu yu mwongo, na baba ya huo.


kwa maana ikiwa Mungu hakuyaachia matawi ya asili, wala hatakuachia wewe.


Yeye asiyemwachilia Mwana wake yeye, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukarimia na vitu vyote pamoja nae?


ijapokuwa malaika, walio wakuu zaidi kwa uwezo na nguvu, hawaleti mashitaka mabaya juu yao mbele ya Bwana.


wala hakuuachilia ulimwengu wa kale, bali alimhifadhi Nuhu, mjumbe wa haki, na watu wengine saba, hapo alipoleta gharika juu ya ulimwengu wa wasiomeha Mungu,


Bwana ajua kuwaokoa wamchao na majaribu, na kuwaweka wasio haki katika hali ya adhabu hatta siku ya hukumu;


afanyae dhambi yu wa Shetani: kwa kuwa Shetani hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihiri, illi azivunje kazi za Shetani.


ni mawimbi ya bahari vasiyozuilika, yakitoa aibu yao wenyewe kama povu, ni nyota zipoteazo, ambao giza ndio akiba yao waliowekewa milele.


Na malaika wasioilinda enzi yao, wakayaacha makao yao, amewaweka kwa hukumu ile kuu katika vifungo vya milele chini ya giza.


Na yule Msingiziaji, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule nyama na yule nabii wa nwongo. Na wataumwa mchana na usiku hatta milele na milele.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo