Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Petro 2:19 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

19 wakiwaahidia uhuru, nao wenyewe ni watumwa wa uharibifu. Maana mtu akishindwa na mtu, huwa mtumwa wa mtu yule.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Huwaahidi watu wengine eti watakuwa huru, kumbe wao wenyewe ni watumwa wa upotovu – maana mtu ni mtumwa wa chochote kile kinachomtawala.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Huwaahidi watu wengine eti watakuwa huru, kumbe wao wenyewe ni watumwa wa upotovu – maana mtu ni mtumwa wa chochote kile kinachomtawala.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Huwaahidi watu wengine eti watakuwa huru, kumbe wao wenyewe ni watumwa wa upotovu — maana mtu ni mtumwa wa chochote kile kinachomtawala.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Wanawaahidi uhuru wakati wao wenyewe ni watumwa wa upotovu; kwa maana “mtu ni mtumwa wa chochote kinachomtawala.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Huwaahidi uhuru hao waliowanasa, wakati wao wenyewe ni watumwa wa ufisadi: kwa maana mtu ni mtumwa wa kitu chochote kinachomtawala.

Tazama sura Nakili




2 Petro 2:19
14 Marejeleo ya Msalaba  

Yesu akawajibu, Amin, amin, nawaambieni, Killa atendae dhambi, ni mtumwa wa dhambi.


Na yule mtu aliyepagawa na pepo akawarukia, akawaweza, akawashinda, hatta wakatoka mbio katika nyumba ile uchi na wamejeruhi.


KRISTO alitufanya huru kwa uhuru; bassi, simameni, msinaswe tena kwa kifungo cha utumwa.


Maana ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali khudumianeni kwa upendo.


wapate tena fahamu zao, na kutoka katika mtego wa Shetani, wamepatikana wahayi nae, hatta kuyafanya apendayo Mungu.


Maana hapo zamani sisi nasi tulikuwa hatuna akili, maasi, tumedanganywa, tukitumikia tamaa na anasa za namna nyingi, tukienenda katika uovu na husuda, tukichukiza na kuchukiana.


kama huru, na wasiontumia uhuru kwa kusetiri ubaya, bali kaina watumwa wa Mungu.


kwa hizo tumekarimiwa ahadi kubwa, za thamani, illi kwa hizo mpate kuwa washirika wa sifa za Mungu, mkiokolewa na ubaribifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa.


Kwa maana wale waliokwisha kuyakimbia machafu ya dunia kwa kumjua sana Bwana, Mwokozi Yesu Kristo, kama wakinaswa tena na kushindwa, hali yao ya mwisho imekuwa mbaya kuliko ile ya kwanza.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo