Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Petro 2:18 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

18 wakinena maneno ya kiburi makuu mno, kwa tamaaza mwili na kwa uasharati huwakhadaa watu waliokwisha kuwakimbia wao waishio katika udanganyifu:

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Husema maneno ya majivuno na yasiyo na maana, na kutumia tamaa zao mbaya za kimwili kuwatega wale ambao wamejitenga hivi karibuni na watu waishio katika udanganyifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 Husema maneno ya majivuno na yasiyo na maana, na kutumia tamaa zao mbaya za kimwili kuwatega wale ambao wamejitenga hivi karibuni na watu waishio katika udanganyifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Husema maneno ya majivuno na yasiyo na maana, na kutumia tamaa zao mbaya za kimwili kuwatega wale ambao wamejitenga hivi karibuni na watu waishio katika udanganyifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Kwa maana wao hunena maneno matupu ya kiburi. Nao wanavutia tamaa mbaya za asili ya mwili, ili kuwashawishi watu ambao wanajiondoa kutoka kwa wale wanaoishi katika hatia.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Kwa maana wao hunena maneno makuu mno ya kiburi cha bure, na kwa kuvutia tamaa mbaya za asili ya mwili, huwashawishi watu ambao ndipo tu wamejiondoa miongoni mwa wale wanaoishi katika ufisadi.

Tazama sura Nakili




2 Petro 2:18
22 Marejeleo ya Msalaba  

Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi.


Na mtu mmoja, jina lake Simon, alikuwa amefanya uchawi katika mji ule tokeapo, akiwashangaza watu wa taifa la Wasamaria, akisema ya kuwa yeye ni mtu mkubwa.


Kama ilivyokhusika na mchana tuenende kwa adabu; si kwa ulafi na ulevi, si kwa ufasiki na uasharati, si kwa ugomvi na wivu.


Bassi nasema neno bili, tena nashuhudu katika Bwana, tangu sasa msienende kama Mataifa waendavyo, katika ubatili wa nia zao,


yule mpingamizi, ajiinuae nafsi yake juu ya killa kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hatta yeye mwenyewe huketi katika hekalu la Mungu, kama Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba ndive Mungu.


Mmefanya anasa katika dunia, na kujifurahisha kwa tamaa; mmejilisha mioyo yenu kama siku ya machinjo.


kwa hizo tumekarimiwa ahadi kubwa, za thamani, illi kwa hizo mpate kuwa washirika wa sifa za Mungu, mkiokolewa na ubaribifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa.


wenye macho yajaayo uzinzi, watu wasiokoma kutenda dhambi, wenye kukhadaa roho zisizo imara, wenye mioyo ilivozoezwa kutamani, wana wa laana;


Na wengi watafuata jeuri zao; kwa hawo njia ya kweli itanenwa unajisi.


Kwa maana wale waliokwisha kuyakimbia machafu ya dunia kwa kumjua sana Bwana, Mwokozi Yesu Kristo, kama wakinaswa tena na kushindwa, hali yao ya mwisho imekuwa mbaya kuliko ile ya kwanza.


akamwokoa Lut, aliyehuzunishwa na mwenendo wa uasharati wa hawo wakhalifu;


Bassi, wapenzi, mkitangulla kujua haya, jilindeni nafsi zenu, msije mkachukuliwa na kosa la hawo wakhalifu, mkaanguka na kuuacha uthubutifu wenu.


ni mawimbi ya bahari vasiyozuilika, yakitoa aibu yao wenyewe kama povu, ni nyota zipoteazo, ambao giza ndio akiba yao waliowekewa milele.


Nikaona nyama mwingine akipanda juu kutoka inchi, nae alikuwa na pembe mbili mfano wa Mwana Kondoo, akanena kama joka.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo