Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Petro 2:17 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

17 Hawa ni visiwa visivyo na maji, na mawingu yachukuliwayo na tufani, ambao weusi wa giza ni akiba waliyowekewa:

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Watu hao ni kama chemchemi zilizokauka, kama mawingu yanayopeperushwa na tufani; makao yao waliyowekewa ni mahali pa giza kuu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Watu hao ni kama chemchemi zilizokauka, kama mawingu yanayopeperushwa na tufani; makao yao waliyowekewa ni mahali pa giza kuu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Watu hao ni kama chemchemi zilizokauka, kama mawingu yanayopeperushwa na tufani; makao yao waliyowekewa ni mahali pa giza kuu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Watu hawa ni chemchemi zisizo na maji, na ukungu unaopeperushwa na tufani. Giza nene limewekwa tayari kwa ajili yao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Watu hawa ni chemchemi zisizo na maji, na ukungu upeperushwao na tufani. Giza nene limewekwa tayari kwa ajili yao.

Tazama sura Nakili




2 Petro 2:17
11 Marejeleo ya Msalaba  

Mfalme akawaambia watumishi, Mfungeni miguu na mikono, mchukueni mkamtupe katika giza la nje: ndiko kutakuwa kilio na kusaga meno.


Na mtumishi yule asiyefaa, mtupeni mbali katika giza ya nje; huko kutakuwa kilio na kusaga meno.


bali wana wa ufalme watatupwa katika giza la nje; ndiko kutakuwa kilio na kusaga meno.


illi tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukulivva kwa killa upepo wa elimu, kwa bila ya watu, kwa ujanja, tukifuata njia za udanganyifu;


Maana hamkufikilia mlima uwezao kuguswa, uliowaka moto, wala wingi jeusi, na giza, na tufani, na mlio wa baragumu na sauti ya maneno;


Kwa maana kama vile Mungu hakuwaachilia malaika waliokosa, bali aliwatupa shimoni, akawatia katika mafungo ya giza, walindwe hatta ije hukumu;


Na malaika wasioilinda enzi yao, wakayaacha makao yao, amewaweka kwa hukumu ile kuu katika vifungo vya milele chini ya giza.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo