Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

2 Petro 2:13 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

13 wakipatwa na madhara, ujira wa udhalimu wao, wakidhani kuwa ulevi wakati wa mchana ni anasa; ni mawaa na aibu, wakifuata anasa katika karamu zao za upendo, wafanyapo karamu pamoja nanyi;

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 na watalipwa mateso kwa mateso ambayo wameyasababisha. Furaha yao ni kufanya, tena mchana kabisa, chochote kinachotosheleza anasa zao za mwili. Hao ni fedheha na aibu tupu kwa jumuiya yenu wakati wanapojiunga nanyi katika karamu zenu, hali wakifurahia njia zao za udanganyifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 na watalipwa mateso kwa mateso ambayo wameyasababisha. Furaha yao ni kufanya, tena mchana kabisa, chochote kinachotosheleza anasa zao za mwili. Hao ni fedheha na aibu tupu kwa jumuiya yenu wakati wanapojiunga nanyi katika karamu zenu, hali wakifurahia njia zao za udanganyifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Watalipwa madhara kwa ajili ya madhara waliyowatendea wengine. Huhesabu kuwa ni fahari kufanya karamu za ulevi na ulafi mchana peupe. Wao ni mawaa na dosari, wakijifurahisha katika anasa zao wanaposhiriki karamu pamoja nanyi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Watalipwa madhara kwa ajili ya madhara waliyowatendea wengine. Huhesabu kuwa ni fahari kufanya karamu za ulevi na ulafi mchana peupe. Wao ni mawaa na dosari, wakijifurahisha katika anasa zao wanaposhiriki katika karamu zenu.

Tazama sura Nakili

2 Petro 2:13
15 Marejeleo ya Msalaba  

Kama ilivyokhusika na mchana tuenende kwa adabu; si kwa ulafi na ulevi, si kwa ufasiki na uasharati, si kwa ugomvi na wivu.

apate kujiletea Kanisa tukufu lisilo na ila ama kunyanzi ama lo lole kama haya; bali liwe takatifu na lisilo na mawaa.

mwisho wao uharibifu, mungu wao tumbo, utukufu wao u katika aibu yao, waniao mambo ya duniani.

Iskander mfua shaba alinionya mabaya mengi; Bwana atamlipa kwa jinsi ya matendo yake.

Mmefanya anasa katika dunia, na kujifurahisha kwa tamaa; mmejilisha mioyo yenu kama siku ya machinjo.

mambo ambayo wao huona kuwa ni ajabu ya ninyi kutokwenda mbio pamoja nao hatta ufisadi usio kiasi, wakiwatukaneni;

walioiacha njia iliyonyoka, wakapotea, wakiifuata njia ya Balaam, mwana wa Bosor, aliyependa ujira wa ndhalimu:

Mlipeni kama yeye alivyolipa, mkamlipe mardufu kwa kadiri ya matendo yake. Katika kikomhe kile alichokichanganisha, mchanganishieni mardufu.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo