Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

2 Petro 2:12 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

12 Lakini hawo kama nyama wasio na akili, kwa asili yao watu wa kukamatwa kama nyama na kupotezwa, wakikufuru katika mambo wasiyoyajua, wataangamizwa katika maangamizo yao;

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Watu hao ambao hutukana chochote kile wasichoelewa, ni sawa na wanyama wasio na akili ambao huzaliwa na baadaye hukamatwa na kuchinjwa! Wataangamizwa kutokana na uharibifu wao wenyewe,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Watu hao ambao hutukana chochote kile wasichoelewa, ni sawa na wanyama wasio na akili ambao huzaliwa na baadaye hukamatwa na kuchinjwa! Wataangamizwa kutokana na uharibifu wao wenyewe,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Watu hao ambao hutukana chochote kile wasichoelewa, ni sawa na wanyama wasio na akili ambao huzaliwa na baadaye hukamatwa na kuchinjwa! Wataangamizwa kutokana na uharibifu wao wenyewe,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Lakini watu hawa hukufuru katika mambo wasiyoyafahamu. Wao ni kama wanyama wasio na akili, viumbe wanaotawaliwa na hisia za mwili, waliozaliwa ili wakamatwe na kuchinjwa. Hawa nao kama wanyama wataangamizwa pia.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Lakini watu hawa hukufuru katika mambo wasiyoyafahamu. Wao ni kama wanyama wasio na akili, viumbe wanaotawaliwa na hisia za mwili, waliozaliwa ili wakamatwe na kuchinjwa. Hawa nao kama wanyama wataangamizwa pia.

Tazama sura Nakili

2 Petro 2:12
17 Marejeleo ya Msalaba  

wizi, uuaji, tamaa mbaya, hila, jeuri, kijicho, matukano, kiburi, upumbafu.

Bassi Yesu akawaambia tena, Mimi naondoka, nanyi mtanitafuta, na mtakufa katika dhambi yenu: niendako mimi, ninyi hamwezi kuja.

Maana yeye apandae kwa mwili wake, katika mwili atavuna uharibifu; bali yeye apandae kwa Roho, katika Roho atavima uzima wa milele.

(Mambo hayo yote huharibika wakati wa kutumiwa), mkifuata maagizo na mafundislio ya wana Adamu?

kwa hizo tumekarimiwa ahadi kubwa, za thamani, illi kwa hizo mpate kuwa washirika wa sifa za Mungu, mkiokolewa na ubaribifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa.

wakiwaahidia uhuru, nao wenyewe ni watumwa wa uharibifu. Maana mtu akishindwa na mtu, huwa mtumwa wa mtu yule.

Lakini watu hawa huyatukana mambo wasiyoyajua, na mambo wayatambuayo kwa asili wajiharibu kwayo kama nyama wasio na akili.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo