Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Petro 2:1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 LAKINI kuliondoka manabii wa uwongo katika watu, kama vile kwenu kutakavyokuwa waalimu wa uwongo, watakaoingiza kwa werevu uzushi wa kupoteza, wakimkana hatta Bwana aliyewanunua, wakijiletea uharibifu nsiokawia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Palitokea manabii wa uongo kati ya watu, na vivyo hivyo waalimu wa uongo watatokea kati yenu. Watu hao wataingiza mafundisho maharibifu na kumkana Bwana aliyewakomboa, na kwa njia hiyo watasababisha ghafla maangamizi yao wenyewe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Palitokea manabii wa uongo kati ya watu, na vivyo hivyo waalimu wa uongo watatokea kati yenu. Watu hao wataingiza mafundisho maharibifu na kumkana Bwana aliyewakomboa, na kwa njia hiyo watasababisha ghafla maangamizi yao wenyewe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Palitokea manabii wa uongo kati ya watu, na vivyo hivyo waalimu wa uongo watatokea kati yenu. Watu hao wataingiza mafundisho maharibifu na kumkana Bwana aliyewakomboa, na kwa njia hiyo watasababisha ghafla maangamizi yao wenyewe.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Lakini pia waliinuka manabii wa uongo miongoni mwa watu, kama watakavyokuwako walimu wa uongo miongoni mwenu. Wataingiza mafundisho yasiyopatana na kweli kwa siri, hata kumkana Bwana Mungu Mwenyezi wa pekee aliyewanunua, na hivyo kujiletea wenyewe maangamizi ya haraka.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Lakini pia waliinuka manabii wa uongo miongoni mwa watu, kama vile watakavyokuwako walimu wa uongo miongoni mwenu. Wataingiza mafundisho yasiyopatana na kweli kwa siri, hata kumkana Isa, Bwana wa pekee aliyewanunua, na hivyo kujiletea wenyewe maangamizi ya haraka.

Tazama sura Nakili




2 Petro 2:1
73 Marejeleo ya Msalaba  

Bali mtu ye yote atakaenikana mbele ya watu, nami nitamkana mbele ya Baba yangu aliye mbinguni.


Na manabii wengi wa uwongo wataondoka, watadanganya wengi.


Kwa maana wataondoka Makristo ya uwongo, na manabii ya uwongo, nao watafanyiza ishara kubwa ua mataajabu; wapate kuwadanganya, kama yumkini, hatta wateule.


Kwa maana wengi watakuja kwa jina langu, wakinena, Mimi ni Kristo; na watadanganya wengi.


Jihadharini na manabii wa uwongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa wa mwitu wakali.


kwa maana wataondoka Makristo wa nwongo, na manabii wa uwongo, watatoa ishara na ajabu, wapate kuwadanganya, kama yumkini, hatta wale wateule.


Nae aliyenikana mbele ya watu, atakanwa mbele za malaika wa Mungu.


Akasema, Jibadharini, msidanganyike; kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakinena, Mimi ndiye, na, Majira yamekaribia. Bassi, msiwafuate hawo.


Ole wenu ninyi, wana Adamu wote watakapowanena vema: maana baba zao waliwatenda manabii ya uwongo mambo kamsi hayo.


Kwa sababu bao ndio wasiomtumikia Bwana wetu Kristo, bali matumbo yao wenyewe; na kwa maneno laini na ya kujipendekeza waidanganya mioyo ya watu wasio wabaya.


kwa maana lazima kuwapo uzushi kwenu, illi waliokubaliwa wawe dhahiri kwenu.


Maana mlinunuliwa kwa thamani. Kwa kuwa ni hivyo, mtukuzeni Mungu kwa mwili wenu, na kwa roho yenu, ambayo ni mali ya Mungu.


Mlinunuliwa kwa thamani; msiwe watumwa wa wana Adamu.


bali kwa ajili ya ndugu za uwongo walioingizwa kwa siri.


Kristo alitukomboa na laana ya sharia, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu: maaua imeandikwa, Amelaaniwa killa mtu atuudikwae juu ya mti:


Wao wawaonea uinyi shauku lakini si kwa vema bali wanataka kuwafungia mlango illi ninyi mwaonee wao shauku.


ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, nzushi,


Katika yeye tuna ukombozi kwa damu yake, masamaha ya dhambi, kwa wingi wa neema yake;


illi tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukulivva kwa killa upepo wa elimu, kwa bila ya watu, kwa ujanja, tukifuata njia za udanganyifu;


mwisho wao uharibifu, mungu wao tumbo, utukufu wao u katika aibu yao, waniao mambo ya duniani.


Mtu asiwanyangʼanye thawabu yenu, akijinyenyekea kwa mapenzi yake mwenyewe tu, na kwa kuwaabudu malaika, akijishughulisha na asiyoyaona, akijivuna burre, kwa akili ya mwili wake,


Angalieni intu asiwateke kwa filosofia yake na madanganya matupu, kwa jinsi ya mapokeo ya wana Adamu, kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu, wala si kwa jinsi ya Kristo.


Lakini mtu asiyewatunza walio wake na khassa watu wa nyumba yake ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko yeye asiyeamini.


Maana ntakuja wakati watakapoikataa elimu yenye uzima; bali kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti,


ambao yapasa wazibwe vinywa vyao. Hawo wanapindua uyumba nzima, wakifundisha yasiyowapasa kwa ajili ya mapato ya aibu.


Mtu mzushi, baada ya kumwonya marra ya kwanza na marra ya pili, mkatae;


Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa nayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho ya neema?


ambae mwampenda, ijapokuwa hamkumwona: ambae ijapokuwa hamwoni sasa, mnamwamini, na kufurahi sana, kwa furaha isiyoneneka, iliyotukuzwa,


Na katika kutamani watajipatia faida kwenu kwa maneno yaliyotungwa: hukumu yao tangu zamani haikawii, wala upotevu wao hausinzii.


Nimewaandikia haya katika khabari za watu wale wanaotaka kuwapoteza.


WAPENZI, msiamini kiila rolio, bali zijaribuni roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uwongo wengi wametokea duniani.


ya kwamba waliwaambia ya kuwa wakati wa mwisho watakuwuko watu wenye kudhihaki, wakizifuata tamaa zao wenyewe zilizo kinyume cha mapenzi ya Mungu.


Kwa maana kuna watu wamejiingiza kwa siri, watu walioandikiwa zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufasiki, nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na Bwana wetu Yesu Kristo.


Nae awakosesha wakaao juu ya inchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya mbele ya nyama, akiwaambia wakaao juu ya inchi kumfanyia sanamu yule nyama aliyekuwa na jeraha ya mauti akaishi.


Napajua ukaapo, ndipo penye kiti cha Shetani: nawe walishika sana jina langu, wala hukuikana imani yangu, hatta katika siku za Antipa shahidi wangu mwaminifu, aliyeuawa kati yenu, hapo akaapo Shetani.


Najua matendo yako na mateso yako na umaskini wako (lakini u tajiri), na matukano yao wasemao ya kuwa ni Wayahudi, nao sio, bali ni sunagogi la Shetani.


Najua matendo yako. Tazama, nimekupa mlango uliofunguliwa mbele yako, wala hapana awezae kuufunga, kwa kuwa unazo nguvu kidogo, nawe ulilitunza neno langu, wala hukulikana jina langu.


Nao waimba uimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulicbinjwa


Wakalia kwa sauti kuu, wakiseina, Ee Mola, Mtakatifu, Mwenye kweli, hatta lini huhukumu na kuipatia haki damu yetu kwao wakaao juu ya inchi?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo