Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Petro 1:9 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

9 Maana yeye asiyekuwa na haya ni kipofu, hawezi kuona vitu vilivyo mbali, amesahau kule kutakaswa dhambi zake za zamani.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Lakini mtu asiye na sifa hizo ni kipofu, hawezi kuona na amesahau kwamba alikwisha takaswa dhambi zake za zamani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Lakini mtu asiye na sifa hizo ni kipofu, hawezi kuona na amesahau kwamba alikwisha takaswa dhambi zake za zamani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Lakini mtu asiye na sifa hizo ni kipofu, hawezi kuona na amesahau kwamba alikwisha takaswa dhambi zake za zamani.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Lakini mtu yeyote asipokuwa na mambo haya, haoni mbali na ni kipofu, naye amesahau kwamba ametakaswa kutoka dhambi zake za zamani.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Lakini mtu yeyote asipokuwa na mambo haya haoni mbali, na ni kipofu, naye amesahau kule kutakaswa kutoka dhambi zake za zamani.

Tazama sura Nakili




2 Petro 1:9
19 Marejeleo ya Msalaba  

Yesu akamkazia macho, akampenda, akamwambia, Umepungukiwa neno moja Enenda, ukauze ulivyo navyo vyote, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni: ukiisha, njoo ukajitwike msalaba wako unifuate.


Yesu aliposikia haya, akamwambia, Neno moja hujalipata bado; viuze vitu vyote ulivyo navyo, ukawagawie maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni. Kiisha, njoo unifuate.


Vivyo hivyo na ninyi jihesabuni kuwa wafu kwa dhambi, na wahayi kwa Mungu katika Kristo Yesu.


Maana ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali khudumianeni kwa upendo.


Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno wala kutokutahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo.


kusudi alitakase na kulisafisha kwa maji, na kwa Neno;


aliyejitoa nafsi yake kwa ajili yetu, illi atuokoe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake, walio na juhudi kwa matendo mema.


bassi si zaidi damu yake Kristo, ambae kwamba kwa Roho ya milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo mawaa, itawasafisheni dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwabudu Mungu aliye hayi?


Mfano wa mambo haya ni ubatizo, nnaowaokoa na ninyi siku hizi; (sio kuwekea, mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamiri safi mbele za Mungu), kwa kufufuka kwake Yesu Kristo;


bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu Kristo, Mwana wake, yatusafisha dhambi zote.


Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u maskini, na mtu wa kuhurumiwa, na mhitaji, na kipofu, na nchi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo