Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Petro 1:21 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

21 Maana unabii haukuletwa zamani kwa mapenzi ya mwana Adamu; hali wana Adamu, watakatifu wa Mungu, walinena, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 Maana hakuna ujumbe wa kinabii unaotokana na matakwa ya binadamu, bali watu walitoa unabii wakiongozwa na Roho Mtakatifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 Maana hakuna ujumbe wa kinabii unaotokana na matakwa ya binadamu, bali watu walitoa unabii wakiongozwa na Roho Mtakatifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 Maana hakuna ujumbe wa kinabii unaotokana na matakwa ya binadamu, bali watu walitoa unabii wakiongozwa na Roho Mtakatifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 Kwa maana unabii haukuja kamwe kwa mapenzi ya mwanadamu, bali watu walinena yaliyotoka kwa Mungu wakiongozwa na Roho Mtakatifu wa Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 Kwa maana unabii haukuja kamwe kwa mapenzi ya mwanadamu, bali watu walinena yaliyotoka kwa Mwenyezi Mungu wakiongozwa na Roho wa Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili




2 Petro 1:21
29 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa sababu Daud mwenyewe alisema, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, Bwana alimwambia Bwana wangu, Keti mkono wangu wa kuume Hatta niwafanyapo adui zako kuwa chini ya miguu yako.


(Kama alivyosema kwa vinywa vya manabii wake watakatifu tangu mwanzo),


Ndugu imepasa andiko litimizwe, alilolinena Roho Mtakatifu zamani kwa kinywa cha Daud, katika khabari za Yuda, aliyekuwa kiongozi wao waliomkamata Yesu: kwa sababu alikuwa amehesabiwa pamoja na sisi,


Na walipokuwa hawapatani wao kwawao, wakaenda zao, Paolo alipokwisha kusema neno hili moja ya kama, Roho Mtakatifu alinena vema na baba zetu, kwa kinywa cha nabii Isaya,


Lakini mambo yale aliyokhubiri Mungu tangu zamani kwa vinywa vya manabii wake wote, ya kama Kristo atateswa, ameyatimiza hivyo.


Na Roho Mtakatifu yatushuhudia; kwa maana, baada ya kunena,


Kwa hiyo, kama anenavyo Robo Mtakatifu, Leo, kama mtasikia sauti yake,


Roho Mtakatifu akionyesha neno hili, ya kwamba njia ya kupaingia patakatifu ilikuwa haijadhihirishwa bado, hapo khema ya kwanza ilipokuwa ingali ikisimama.


wakitafuta ni wakati upi, na wakati wa namna gani ulioonywa na Roho ya Kristo iliyokuwa ndaui yao, aliyetangulia kuyashuhudia mateso yatakayompata Kristo, na utukufu utakaokuwa baada ya hayo.


Nikaanguka mbele ya miguu yake, nimsujudie, akaniambia, Angalia, usifanye hivi: mimi mjoli wako na mmoja wa ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Msujudu Mungu: kwa maana ushuhuda wa Yesu ni roho ya unabii.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo