Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




2 Petro 1:19 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

19 Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa ingʼaayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya assubuhi kuzuka mioyoni mwenu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Tena, ujumbe wa manabii watuthibitishia jambo hilo; nanyi mwafanya vema kama mkiuzingatia, maana ni kama taa inayoangaza mahali penye giza mpaka siku ile itakapopambazuka na mwanga wa nyota ya asubuhi utakapong'ara mioyoni mwenu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Tena, ujumbe wa manabii watuthibitishia jambo hilo; nanyi mwafanya vema kama mkiuzingatia, maana ni kama taa inayoangaza mahali penye giza mpaka siku ile itakapopambazuka na mwanga wa nyota ya asubuhi utakapong'ara mioyoni mwenu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Tena, ujumbe wa manabii watuthibitishia jambo hilo; nanyi mwafanya vema kama mkiuzingatia, maana ni kama taa inayoangaza mahali penye giza mpaka siku ile itakapopambazuka na mwanga wa nyota ya asubuhi utakapong'ara mioyoni mwenu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Nasi tunalo pia neno la hakika zaidi la unabii, ambalo mtafanya vyema mkiliangalia kwa bidii, kama nuru inavyong’aa gizani, hadi kupambazuke na nyota ya asubuhi izuke mioyoni mwenu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Nasi tunalo pia neno la hakika zaidi la unabii, ambalo mtafanya vyema mkiliangalia kwa bidii, kama vile nuru inavyong’aa gizani, hadi kupambazuka na nyota ya asubuhi izuke mioyoni mwenu.

Tazama sura Nakili




2 Petro 1:19
27 Marejeleo ya Msalaba  

Watu waliokaa gizani Waliona mwanga mkuu, Nao waliokaa katika inchi na kivuli cha mauti, Mwanga umewazukia.


Yeye alikuwa taa iwakayo na kuangaza, na ninyi mlipenda kuishangilia nuru yake kitambo.


Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake: na hayo ndiyo yanayonishuhudia:


Bassi Yesu akanena nao tena, akisema. Mimi ni nuru ya ulimwengu; anifuatae hatakwenda katika giza kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.


mjiepushe na vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, na nyama zilizosongwa, na asharati. Mkijizuia na hayo, mtafanya vema. Salamu.


Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa Thessaloniki, kwa kuwa walilipokea Neno kwa uelekefu wa moyo, wakayachunguza maandiko, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo.


Kwa maana, ikiwa lile neno lililonenwa na malaika lilikuwa imara, na killa kosa na uasi ulipata ujira wa haki,


Illakini mkiitimiza sharia ya kifalme kama ilivyoandikwa. Mpende jirani yako kama nafsi yako, mwatenda vyema.


Katika khabari ya wokofu huo walitafutatafuta na kuchunguzachunguza manabii waliotabiri khabari va neema itakayowafikia,


Amwaminiye Mwana wa Mungu anao ushuhuda ndani yake. Asiyemwamini Mungu amemfanya kuwa mwongo, kwa kuwa hakuuamini ushuhuda ambao Mungu amemsbuhudia Mwana wake.


waliokushuhudia upendo wako mbele ya kanisa; utafanya vizuri ukiwasafirisha kam a ilivyo wajibu wako kwa Mungu.


Nami nitampa nyota ya assubuhi.


Mimi Yesu nalimtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzao wa Daud, ile nyota yenye kungʼaa ya assubuhi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo