Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Yohana 5:4 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

4 Kwa maana killa kitu kilihozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, imani yetu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 maana kila aliye mtoto wa Mungu anaweza kuushinda ulimwengu. Hivi ndivyo tunavyoushinda ulimwengu: Kwa imani yetu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 maana kila aliye mtoto wa Mungu anaweza kuushinda ulimwengu. Hivi ndivyo tunavyoushinda ulimwengu: Kwa imani yetu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 maana kila aliye mtoto wa Mungu anaweza kuushinda ulimwengu. Hivi ndivyo tunavyoushinda ulimwengu: kwa imani yetu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Kwa maana kila aliyezaliwa na Mungu huushinda ulimwengu. Huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, yaani hiyo imani yetu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Kwa maana kila aliyezaliwa na Mwenyezi Mungu huushinda ulimwengu. Huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, yaani, hiyo imani yetu.

Tazama sura Nakili




1 Yohana 5:4
21 Marejeleo ya Msalaba  

waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.


Haya nimewaambieni, mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mtapata shidda: lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.


Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa marra ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.


Lakini tumshukuru Mungu atupae kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo.


Kama mkijua ya kuwa yeye ni mwenye haki, jueni ya kuwa killa atendae haki amezaliwa nae.


Killa mtu aliyezaliwa na Mungu hafanyi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kufanya dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu.


Ninyi, watoto wangu, mwatokana na Mungu: nanyi mmewashinda, kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia.


KILLA mtu aaminiye kwamba Yesu ni Kristo amezaliwa na Mungu. Na killa mtu ampendae mwenye kuzaa ampenda na yeye mwenye kuzaliwa nae.


Twajua ya kuwa killa mtu aliyezaliwa na Mungu hakosi: bali yeye aliyezaliwa na Mungu ajilinda, na yule mwovu hamgusi.


Mwenye kuushinda ulimwengu ni nani, isipokuwa yeye aaminiye ya kwamba Yesu yu Mwana wa Mungu?


Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; wala hawakupenda maisha yao hatta wakati wa kufa.


Nikaona kama mfano wa bahari ya kioo iliyochangamana na moto, nao wenye kushinda, na kujiepusha na yule nyama na sanamu yake na alama yake, na hesabu ya jina lake, wamesimama juu ya bahari ya kioo, wenye vinubi vya Mungu.


Yeye aliye na sikio na asikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindae hatapatikana na madhara ya mauti ya pili.


Yeye aliye na sikio na asikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindae nitampa kula baadhi ya ile manna iliyofiehwa, nami nitampa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina, jina asilolijua mtu illa yeye aliyepewa.


Na yeye ashindae na kuyatunza matendo yangu hatta mwisho, nitampa mamlaka juu ya mataifa,


Yeye alive na sikio, na asikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindae, nitampa kula matunda ya mti wa uzima ulio kati kati va bustani ya Mungu.


Yeye ashindae, nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu wangu, Yerusalemi ulio mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe, lile jipya.


Yeye asbindae, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda, nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.


Yeye ashindae atavikwa mavazi meupe, wala sitalifuta jina lake katika kitabu cha uzima, nami nitaliungama jina lake mbele za Baba yaugu, na mbele ya malaika zake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo