Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Yohana 5:1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 KILLA mtu aaminiye kwamba Yesu ni Kristo amezaliwa na Mungu. Na killa mtu ampendae mwenye kuzaa ampenda na yeye mwenye kuzaliwa nae.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Kila mtu anayeamini kwamba Yesu ni Kristo, huyo ni mtoto wa Mungu. Kila anayempenda mzazi humpenda pia mtoto wa huyo mzazi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Kila mtu anayeamini kwamba Yesu ni Kristo, huyo ni mtoto wa Mungu. Kila anayempenda mzazi humpenda pia mtoto wa huyo mzazi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Kila mtu anayeamini kwamba Yesu ni Kristo, huyo ni mtoto wa Mungu. Kila anayempenda mzazi humpenda pia mtoto wa huyo mzazi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Kila mtu anayeamini kwamba Isa ndiye Al-Masihi amezaliwa na Mungu, na yeyote ampendaye Baba humpenda pia mtoto aliyezaliwa naye.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Kila mtu anayeamini kwamba Isa ndiye Al-Masihi amezaliwa na Mungu, na yeyote ampendaye Baba humpenda pia mtoto aliyezaliwa naye.

Tazama sura Nakili




1 Yohana 5:1
27 Marejeleo ya Msalaba  

Simon Petro akajibu, akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hayi.


ya kama, Astahili umtendee neno hili, maana apenda taifu letu, nae alitujengea sunagogi letu.


Vyote vyalifanyika kwa huyu. Wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.


Anichukiae mimi, humchukia na Baba yangu.


Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa marra ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.


Nasi tumeamini, tena tumejua ya kuwa wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hayi.


Yesu akawaambia, Kama Mungu angekuwa baba yenu mngenipenda mimi; kwa maana nalitoka kwa Mungu, na nimekuja; wala sikuja kwa nafsi yangu, bali yeye ndiye aliyenituma.


Wakawa wakiendelea njiani, wakafika mahali penye maji: yule tawashi akasema, Yanizuia nini nisibatizwe?


Filipo akasema, Ukiamini kwa moyo wako wote, ni halali. Akajibu, akanena, Namwamini Mwana wa Mungu kuwa ndiye Yesu Kristo.


Alipopenda alituzaa sisi kwa neno la kweli, tuwe kama limhuko la viumbe vyake.


Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambae kwa rehema zake nyingi alituzaa marra ya pili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuliwa kwake Yesu Kristo,


Yeye ampendae ndugu yake, akaa katika nuru, wala ndani yake hamna kikwazo.


Kama mkijua ya kuwa yeye ni mwenye haki, jueni ya kuwa killa atendae haki amezaliwa nae.


Sisi tunajua ya kuwa tumepita toka mauti hatta uzima, kwa maana twawapenda ndugu. Asiyependa, akaa katika mauti.


Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia hii, akamwona ndugu yake yu muhitaji, akamzuilia huruma zake, je! huko ndiko kumpenda Mungu?


Killa mtu aliyezaliwa na Mungu hafanyi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kufanya dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu.


Hivi mwaijua Roho ya Mungu; killa roho iungamayo kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatokana na Mungu.


Mtu akisema, Nampenda Mungu, nae anamchukia ndugu yake, yu mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambae amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambae hakumwona.


Wapenzi, tupendane: kwa kuwa pendo ni la Mungu, na killa apendae amezaliwa na Mungu, nae anamjua Mungu.


Twajua ya kuwa killa mtu aliyezaliwa na Mungu hakosi: bali yeye aliyezaliwa na Mungu ajilinda, na yule mwovu hamgusi.


Kwa maana killa kitu kilihozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, imani yetu.


Mwenye kuushinda ulimwengu ni nani, isipokuwa yeye aaminiye ya kwamba Yesu yu Mwana wa Mungu?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo