Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Yohana 4:9 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

9 Hivi pendo la Mungu lilionekana kwetu, kwa kuwa Mungu amempeleka Mwana wake pekee ulimwenguni, tupate uzima kwa yeye.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Na Mungu alionesha upendo wake kwetu kwa kumtuma Mwanae wa pekee ulimwenguni, ili tuwe na uhai kwa njia yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Na Mungu alionesha upendo wake kwetu kwa kumtuma Mwanae wa pekee ulimwenguni, ili tuwe na uhai kwa njia yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Na Mungu alionesha upendo wake kwetu kwa kumtuma Mwanae wa pekee ulimwenguni, ili tuwe na uhai kwa njia yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Hivi ndivyo Mungu alivyoonesha pendo lake kwetu: Mungu alimtuma Mwanawe wa pekee ulimwenguni, ili tupate uzima kupitia kwake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Hivi ndivyo Mungu alivyoonyesha pendo lake kwetu: Mwenyezi Mungu alimtuma Mwanawe wa pekee ulimwenguni, ili tupate uzima kupitia kwake.

Tazama sura Nakili




1 Yohana 4:9
27 Marejeleo ya Msalaba  

Bassi alikuwa na mwana mmoja bado, mpendwa wake; huyu nae akamtuma kwao wa mwisho, akinena, Watamjali mwana wangu.


Roho ya Bwana ni juu yangu, Kwa sababu amenitia mafuia kuwakhubiri maskini khabari njema. Amenituma kuwaponya waliopondeka moyo, Kuwatangazia wafungwa kufunguliwa, na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha wa huru waliosetwa,


Mwizi haji illa aibe, achinje, aharibu; mimi nalikuja wawe na uzima, na wawe nao tele.


Yesu akamwambia, Ndimi niliye njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba bila kwa mimi.


Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hatta akampeleka Mwana wake wa pekee, illi mtu aliye yote amwaminiye asipotee, bali apate uzima wa milele.


Amwaminiye hahukumiwi; asiyemwamini amekwisha kuhukumiwa, kwa maana hakuliamini jina la Mwana wa pekee wa Mungu.


illi wote wamheshimu Mwana kama wanavyomheshimu Baba. Asiyemheshimu Mwana, hamheshimu Baba aliyempeleka.


Yesu akajibu, akawaambia, Hii ni kazi ya Mungu, mmwamini yeye aliyetumwa nae.


Mimi ni mkate wa uzima ulioshuka kutoka mbinguni; mtu akila mkate huu, ataishi milele: na mkate nitakaotoa mimi ni nyama yangu nitakayotoa kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.


Kama vile Baba aishiye alivyonituma mimi, nami naishi kwa ajili ya Baba, kadhalika yeye nae anilae ataishi kwa ajili yangu.


Nae aliyenipeleka yu pamoja nami; Baba hakuniacha peke yangu: kwa sababu mimi nafanya siku zote yampendezayo.


Yesu akawaambia, Kama Mungu angekuwa baba yenu mngenipenda mimi; kwa maana nalitoka kwa Mungu, na nimekuja; wala sikuja kwa nafsi yangu, bali yeye ndiye aliyenituma.


Yesu akajibu, Huyu hakutenda dhambi wala wazazi wake; bali kazi za Mungu zidhihirishwe kwake.


Yeye asiyemwachilia Mwana wake yeye, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukarimia na vitu vyote pamoja nae?


Kwa maana alimwambia malaika yupi wakati wo wote, Mwana wangu ndiwe, mimi leo nimekuzaa? na tena, Mimi nitakuwa kwake baba, na yeye kwangu mwana?


Hivi tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliweka maisha yake kwa ajili yetu; imetupasa na sisi kuweka maisha yetu kwa ajili ya ndugu.


Hili ndilo pendo, si kwamba sisi twalimpenda Mungu, bali kwamba yeye alitupenda sisi, akampeleka Mwana wake kuwa kipatanislio kwa dhambi zetu.


Na sisi tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu ndani yetu na kuliamini. Mungu ni pendo, nae akaae katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake.


Na huu ndio ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika Mwana wake.


Nimewaandikia mambo haya, illi mjue ya kuwa mna uzima wa milele, ninyi mnaoliamini Jina la Mwana wa Mungu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo