Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Yohana 4:20 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

20 Mtu akisema, Nampenda Mungu, nae anamchukia ndugu yake, yu mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambae amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambae hakumwona.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

20 Mtu akisema kwamba anampenda Mungu, hali anamchukia ndugu yake, huyo ni mwongo. Maana mtu asiyempenda ndugu yake ambaye anamwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hamwoni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

20 Mtu akisema kwamba anampenda Mungu, hali anamchukia ndugu yake, huyo ni mwongo. Maana mtu asiyempenda ndugu yake ambaye anamwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hamwoni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

20 Mtu akisema kwamba anampenda Mungu, hali anamchukia ndugu yake, huyo ni mwongo. Maana mtu asiyempenda ndugu yake ambaye anamwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hamwoni.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

20 Ikiwa mtu atasema, “Nampenda Mungu,” lakini anamchukia ndugu yake, yeye ni mwongo. Kwa maana kila mtu asiyempenda ndugu yake ambaye anamwona, atampendaje Mungu asiyemwona?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

20 Ikiwa mtu atasema, “Nampenda Mwenyezi Mungu,” lakini anamchukia ndugu yake, yeye ni mwongo. Kwa maana kila mtu asiyempenda ndugu yake ambaye anamwona, atampendaje Mungu asiyemuona?

Tazama sura Nakili




1 Yohana 4:20
9 Marejeleo ya Msalaba  

Hivi watu wote watajua ya kuwa m wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi.


ambae mwampenda, ijapokuwa hamkumwona: ambae ijapokuwa hamwoni sasa, mnamwamini, na kufurahi sana, kwa furaha isiyoneneka, iliyotukuzwa,


Tukisema twashirikiana nae, tena tukienenda gizani, twasema uwongo, wala hatuifanyi iliyo kweli;


Tukisema hatuna dhambi, twajidanganya, wala kweli haimo mwetu.


Bali yeye amchukiae ndugu yake, yu katika giza, tena anakwenda katika giza, wala hajui aendako, kwa sababu giza imempofusha macho.


Yeye asemae, Nimemjua, nae hazishiki amri zake, ni mwongo, na kweli haimo ndani yake.


Yeye asemae kwamba yumo katika nuru, nae amchukia ndugu yake, yumo gizani hatta sasa.


Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia hii, akamwona ndugu yake yu muhitaji, akamzuilia huruma zake, je! huko ndiko kumpenda Mungu?


Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote. Tukipendana, Mungu hukaa ndani yetu, na pendo limekamilishwa ndani yetu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo