Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Yohana 3:9 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

9 Killa mtu aliyezaliwa na Mungu hafanyi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kufanya dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Kila aliye mtoto wa Mungu hatendi dhambi, maana anayo hali ya kimungu ndani yake; hawezi kutenda dhambi kwa sababu yeye ni mtoto wa Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Kila aliye mtoto wa Mungu hatendi dhambi, maana anayo hali ya kimungu ndani yake; hawezi kutenda dhambi kwa sababu yeye ni mtoto wa Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Kila aliye mtoto wa Mungu hatendi dhambi, maana anayo hali ya kimungu ndani yake; hawezi kutenda dhambi kwa sababu yeye ni mtoto wa Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Yeyote aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wa Mungu wakaa ndani yake, wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa na Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Yeyote aliyezaliwa na Mwenyezi Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wa Mungu wakaa ndani yake, wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa na Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili




1 Yohana 3:9
18 Marejeleo ya Msalaba  

Mti mwema hauwezi kuzaa matunda hafifu, wala mti uliopea kuzaa matunda mazuri.


waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.


Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa marra ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.


Kwamba ni haki mbele za Mungu kuwasikiliza ninyi kuliko Mungu, hukumuni ninyi wenyewe; maana sisi hatuwezi kuacha kuyanena mambo tuliyoyaona na kuyasikia.


Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi?


Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho hushindana na mwili; kwa maana liizi zimepingana, hatta hamwezi kufanya nmayotaka.


katika tumaini la nzima wa milele, ambao Mungu asiyeweza kusema nwongo aliuahidi kabla ya nyakati za zamani;


kwa kuwa mmezaliwa marra ya pili, si kwa mbegu iharibikayo, bali isiyoharibika, kwa neno la Mungu lenye uzima, na lidumulo hatta milele.


Kama mkijua ya kuwa yeye ni mwenye haki, jueni ya kuwa killa atendae haki amezaliwa nae.


Killa akaae ndani yake batendi dhambi; killa atendae dhambi bakumwona, wala hakumtambua.


Wapenzi, tupendane: kwa kuwa pendo ni la Mungu, na killa apendae amezaliwa na Mungu, nae anamjua Mungu.


KILLA mtu aaminiye kwamba Yesu ni Kristo amezaliwa na Mungu. Na killa mtu ampendae mwenye kuzaa ampenda na yeye mwenye kuzaliwa nae.


Twajua ya kuwa killa mtu aliyezaliwa na Mungu hakosi: bali yeye aliyezaliwa na Mungu ajilinda, na yule mwovu hamgusi.


Kwa maana killa kitu kilihozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, imani yetu.


Mpenzi, usiuige ubaya, bali wema. Yeye atendae mema ni wa Mungu, bali yeye atendae mabaya hakumwona Mungu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo