Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Yohana 3:23 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

23 Na hii ndiyo amri yake, tuliamini jina la Mwana wake Yesu Kristo, na kupendana, kama alivyotupa amri.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

23 Na, amri yake ndiyo hii: Kumwamini Mwanae Yesu Kristo, na kupendana kama alivyotuamuru.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

23 Na, amri yake ndiyo hii: Kumwamini Mwanae Yesu Kristo, na kupendana kama alivyotuamuru.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

23 Na, amri yake ndiyo hii: Kumwamini Mwanae Yesu Kristo, na kupendana kama alivyotuamuru.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

23 Hii ndiyo amri yake: kwamba tuliamini Jina la Mwanawe, Isa Al-Masihi, na kupendana sisi kwa sisi kama yeye alivyotuamuru.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

23 Hii ndiyo amri yake: kwamba tuliamini Jina la Mwanawe, Isa Al-Masihi, na kupendana sisi kwa sisi kama yeye alivyotuamuru.

Tazama sura Nakili




1 Yohana 3:23
24 Marejeleo ya Msalaba  

Na ya pili yafanana nayo, ndiyo hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako.


Likawako wingu, likawatia uvuli: sauti ikatoka katika lile wingu, Huyu ui Mwana wangu, mpendwa wangu, msikieni yeye.


Bali wote waliompokea aliwapa mamlaka ya kufanyika watoto wa Mungu, ndio waliaminio jina lake:


Amri mpya nawapeni, mpendane; kama vile nilivyowapenda ninyi, na ninyi mpendane vivyo hivyo.


MSIFADHAIKE mioyo yenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi.


Amri yangu ndio hii, mpendane, kama nilivyowapenda ninyi.


Na uzima wa milele ni huu, wakujue wewe, Mungu wa peke yake, wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.


Hatta alipokuwapo Yerusalemi wakati wa Pasaka katika siku kuu, watu wengi wakaliamini jina lake, wakiona ishara zake alizozifanya.


Amwaminiye hahukumiwi; asiyemwamini amekwisha kuhukumiwa, kwa maana hakuliamini jina la Mwana wa pekee wa Mungu.


Yesu akajibu, akawaambia, Hii ni kazi ya Mungu, mmwamini yeye aliyetumwa nae.


Wakamwambia, Mwamini Bwana Yesu Kristo, nawe utaokoka pamoja na uyumba yako.


mkaenende katika upendo, kama na Kristo alivyowapenda ninyi, akajitoa kwa ajili yetu, sadaka na dhabihu kwa Mungu, kuwa harufu nzuri.


Kwa khabari ya upendano, hamna haja niwaandikie: maana ninyi wenyewe mmefundishwa na Mungu kupendana.


Ni neno la kuaminiwa, listahililo kukubaliwa na watu wote, ya kwamba Kristo Yesu alikuja ulimwenguni, awaokoe wenye dhambi; na mimi wa kwanza wao.


Mkiisha kujisafisha roho zenu kwa kuitii kweli, kwa Roho, kiasi cha kuufikilia upendano usio na unafiki, bassi jitahidini kupendana kwa moyo;


zaidi ya yote mwe na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husetiri wingi wa dhambi;


Ndugu, siwaandikii amri mpya, illa amri ya zamani mliyokuwa nayo tangu mwanzo.


Maana hii ndiyo khabari tuliyosikia tangu mwanzo, tupendane sisi kwa sisi;


Killa aungamae ya kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu, Mungu hukaa ndani yake, nae ndani ya Mungu.


Na amri hii tumepewa nae, ya kwamba yeye ampendae Mungu, ampende na ndugu yake.


Nimewaandikia mambo haya, illi mjue ya kuwa mna uzima wa milele, ninyi mnaoliamini Jina la Mwana wa Mungu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo