Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Yohana 3:22 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

22 na lo lote tuombalo, twalipokea kwake, kwa kuwa twazishika amri zake, na kuyatenda yapendezayo machoni pake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

22 na kupokea kwake chochote tunachoomba, maana tunazitii amri zake na kufanya yale yanayompendeza.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

22 na kupokea kwake chochote tunachoomba, maana tunazitii amri zake na kufanya yale yanayompendeza.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

22 na kupokea kwake chochote tunachoomba, maana tunazitii amri zake na kufanya yale yanayompendeza.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

22 lolote tuombalo, twalipokea kutoka kwake, kwa sababu tumezitii amri zake na kutenda yale yanayompendeza.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

22 lolote tuombalo, twalipokea kutoka kwake, kwa sababu tumezitii amri zake na kutenda yale yanayompendeza.

Tazama sura Nakili




1 Yohana 3:22
37 Marejeleo ya Msalaba  

Alipokuwa akisema, wingu jeupe likawatia uvuli; sauti ikatoka katika lile wingu, ikinena, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, niliyependezwa nae; msikieni yeye.


Na yo yote mtakayoyaomba katika kusali, mkiamini, mtapokea.


Kwa sababu biyo nawaambieni, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea nayo yatakuwa yenu.


Na mkiomba lo lote kwa jina langu, hili nitalifanya, Baba atukuzwe ndani ya Mwana.


Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; kama mimi nilivyozishika amri za Baba yangu, na kukaa katika pendo lake.


Mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, mtaomba killa mtakalo, na mtafanyiziwa.


Yesu akajibu, akawaambia, Hii ni kazi ya Mungu, mmwamini yeye aliyetumwa nae.


Nae aliyenipeleka yu pamoja nami; Baba hakuniacha peke yangu: kwa sababu mimi nafanya siku zote yampendezayo.


Twajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi: bali mtu akiwa mcha Mungu, na kufanya mapenzi yake, huyo amsikia.


Bassi zamani zile za ujinga Mungu alijifanya kama hauoni; bali sasa anawakhuhiri watu wote wa killa mahali watubu.


nikiwashuhudia Wayahudi na Wayunani toba iliyo kwa Mungu, na imani iliyo kwa Bwana wetu Yesu Kristo.


Lakini ninavyo vitu vyote na kuzidi; tena nimejaa tele, nimepokea kwa mkono ya Epafrodito vitu vile vilivyotoka kwenu, harufu ya manukato, sadaka yenye kibali, impendezayo Mungu.


mwenende kama ilivyo wajib wenu kwa Bwana, mkimpendeza kabisa; kwa killa kazi njema mkizaa matunda, mkizidi katika maarifa ya Mungu;


awafanye kuwa wrakamilifu katika killa tendo jema, mpate kuyafanya mapenzi yake, nae akifanya ndani yetu lipendezalo mbele zake, kwa Yesu Kristo; utukufu una yeye milele na milele. Amin.


Lakini mtu wa kwemi akipungukiwa hekima, aombe dua kwa Mungu, awapae wote kwa ukarimu, wala hakemei; nae atapewa.


Mwaomba wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, illi mvilumie kwa tamaa zenu.


Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.


Na hivi twajua ya kuwa tumemjua, ikiwa tunashika amri zake.


Na huu ndio njasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu kama vile apendavyo, atusikia:


Tufuate:

Matangazo


Matangazo