Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Yohana 3:15 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

15 Killa amchukiae ndugu yake ni mwuaji: nti mnajua ya kuwa mwuaji bana uzima wa milele ukikaa ndani yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Kila anayemchukia ndugu yake ni muuaji; nanyi mnajua kwamba muuaji yeyote yule hana uhai wa milele ndani yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Kila anayemchukia ndugu yake ni muuaji; nanyi mnajua kwamba muuaji yeyote yule hana uhai wa milele ndani yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Kila anayemchukia ndugu yake ni muuaji; nanyi mnajua kwamba muuaji yeyote yule hana uhai wa milele ndani yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Yeyote amchukiaye ndugu yake ni muuaji, nanyi mwajua kwamba muuaji hana uzima wa milele ndani yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Yeyote amchukiaye ndugu yake ni muuaji, nanyi mwajua ya kwamba muuaji hana uzima wa milele ndani yake.

Tazama sura Nakili




1 Yohana 3:15
19 Marejeleo ya Msalaba  

Bali mimi miwaambieni, Killa mtu atazamae mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini nae moyoni mwake.


Bassi yule Herodias akawa akimvizia, akataka kumwua, asipate.


walakini ye yote atakaekunywa maji yale nitakayompa mimi, hataona kiu milele, bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujika hatta uzima wa milele.


Ninyi wa baba yenu Shetani, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzifanya. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo, wala hakusimama katika kweli kwa kuwa kweli hamna ndani yake. Asemapo uwongo, husema yaliyo yake mwenyewe, kwa sababu yu mwongo, na baba ya huo.


Kulipopambazuka, baadhi ya Wayahudi wakafanya mapatano, wakajifunga kwa kiapo wakisema. Hatuli wala hatunywi hatta tutakapokwisha kumwua Paolo.


Nao wakaenda kwa makuhani wakuu na wazee, wakasema, Tumejifunga kwa kiapo, tusionje kitu hatta tutakapomwua Paolo.


Khalafu ile tamaa ikiisha kuchuikua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti.


kwa kuwa mmezaliwa marra ya pili, si kwa mbegu iharibikayo, bali isiyoharibika, kwa neno la Mungu lenye uzima, na lidumulo hatta milele.


Bali yeye amchukiae ndugu yake, yu katika giza, tena anakwenda katika giza, wala hajui aendako, kwa sababu giza imempofusha macho.


Yeye asemae kwamba yumo katika nuru, nae amchukia ndugu yake, yumo gizani hatta sasa.


Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, nae waabuduo sanamu, na wawongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndio mauti ya pili.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo