Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Yohana 3:12 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

12 si kama Kain alivyokuwa wa yule Mwovu, akamwua ndugu yake. Nae alimwua kwa sababu gani? Kwa sababu matendo yake yalikuwa mabaya, na ya ndugu yake ya haki.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Tusiwe kama Kaini ambaye, kwa kuongozwa na yule Mwovu, alimuua ndugu yake. Na, kwa nini alimuua? Kwa sababu matendo yake yalikuwa maovu, lakini yale ya ndugu yake yalikuwa mema!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Tusiwe kama Kaini ambaye, kwa kuongozwa na yule Mwovu, alimuua ndugu yake. Na, kwa nini alimuua? Kwa sababu matendo yake yalikuwa maovu, lakini yale ya ndugu yake yalikuwa mema!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Tusiwe kama Kaini ambaye, kwa kuongozwa na yule Mwovu, alimuua ndugu yake. Na, kwa nini alimuua? Kwa sababu matendo yake yalikuwa maovu, lakini yale ya ndugu yake yalikuwa mema!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Msiwe kama Kaini aliyekuwa wa yule mwovu akamuua ndugu yake. Basi kwa nini alimuua? Ni kwa sababu matendo yake Kaini yalikuwa mabaya na ya ndugu yake yalikuwa ya haki.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Msiwe kama Kaini aliyekuwa wa yule mwovu akamuua ndugu yake. Basi kwa nini alimuua? Ni kwa sababu matendo yake Kaini yalikuwa mabaya na ya ndugu yake yalikuwa ya haki.

Tazama sura Nakili




1 Yohana 3:12
31 Marejeleo ya Msalaba  

Killa alisikiae neno la ufalme asifahamu, huja yule mwovu, akaliteka lililopandwa moyoni mwake. Huyu ndiye aliyepandwa njiani.


na lile konde ni ulimwengu; na zile mbegu njema ni wana wa ufalme; na yale magugu ni wana wa yule mwovu;


illi iwajieni damu yote ya haki iliyomwagika katika inchi, tangu damu ya Habil, yule mwenye haki, hatta damu ya Zakaria, mwana wa Barakia, mliyemwua kati ya patakatifu na madhbahu,


Liwali akasema, Kwani? ubaya gani alioutenda? Wakazidi sana kupiga kelele, wakinena, Asulibiwe.


Bali maneno yenu yawe, Ndio, ndio; Sio, sio: kwa kuwa izidiyo haya yatoka kwa yule mwovu.


tangu damu ya Habil hatta damu ya Zakaria aliyeuawa kati ya madhhahu na patakatifu. Naam, nawaambieni, itatakwa kwa kizazi hiki.


Yesu akawajibu, Kazi njema nyingi nimewaonyesha zitokazo kwa Baba yangu: katika kazi hizo ni ipi mnayonipigia mawe?


Lakini sasa mnatafuta kuniua mimi, mtu niliyewaambia kweli ile niliyoisikia kwa Baba yangu. Ibrahimu hakufanya hivi. Ninyi nmazitenda kazi za baba yenu.


Wakamwambia, Sisi hatukuzaliwa kwa zina; tuna baba mmoja, yaani Mungu.


Ni yupi katika manabii ambae baba zenu hawakumwudhi? nao waliwaua wale waliotabiri khabari za kuja kwake yule mwenye haki; ambae ninyi sasa mmemsaliti mkamwua;


Maana uinyi, ndugu, mlikuwa wafuasi wa makanisa ya Mungu yaliyo katika Yahudi, katika Kristo Yesu; kwa kuwa mlipata mateso yale yale kwa watu wa taifa lenu, waliyopata na hao kwa Wayahudi;


Kwa imani Habil alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko Kain; kwa hiyo alishuhudiwa kuwa ana haki; Mungu akazishuhudia sadaka zake, na kwa hiyo ijapokuwa amekufa, angali akinena.


na Yesu mwenye kuleta agano jipya, na damu ya kunyunyizwa inenayo mema kuliko ile ya Habil.


mambo ambayo wao huona kuwa ni ajabu ya ninyi kutokwenda mbio pamoja nao hatta ufisadi usio kiasi, wakiwatukaneni;


afanyae dhambi yu wa Shetani: kwa kuwa Shetani hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihiri, illi azivunje kazi za Shetani.


Ole wao! kwa sababu walikwenda katika njia ya Kain, na kulifuata kosa la Balaam pasipo kujizuia, kwa ajili ya ujira, nao wameangamia katika maasi ya Kora.


Nikamwona yule mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu, na kwa damu ya mashahidi wa Yesu. Nami nilipomwona nikastaajabu ajabu kuu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo