Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Yohana 3:1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 FAHAMUNI, ni pendo la nanma gani alilotupa Baba, kuitwa wana wa Mungu. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Oneni, basi, jinsi Baba alivyotupenda mno hata tunaitwa watoto wa Mungu! Na kweli, ndivyo tulivyo. Ndiyo maana ulimwengu haututambui sisi, kwani haumjui Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Oneni, basi, jinsi Baba alivyotupenda mno hata tunaitwa watoto wa Mungu! Na kweli, ndivyo tulivyo. Ndiyo maana ulimwengu haututambui sisi, kwani haumjui Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Oneni, basi, jinsi Baba alivyotupenda mno hata tunaitwa watoto wa Mungu! Na kweli, ndivyo tulivyo. Ndiyo maana ulimwengu haututambui sisi, kwani haumjui Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Tazameni ni pendo kuu namna gani alilotupatia Baba, kwamba sisi tuitwe wana wa Mungu! Na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Tazameni ni pendo kuu namna gani alilotupa Baba, kwamba sisi tuitwe wana wa Mwenyezi Mungu! Na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye.

Tazama sura Nakili




1 Yohana 3:1
33 Marejeleo ya Msalaba  

kwa kuwa hawawezi kufa tena, maana huwa sawasawa na malaika; tena ni wana wa Mungu kwa kuwa wana wa ule ufufuo.


Bali wote waliompokea aliwapa mamlaka ya kufanyika watoto wa Mungu, ndio waliaminio jina lake:


wala si kwa ajili ya taifa lile tu, lakini pamoja na haya awakusanye watoto wa Mungu waliotawanyika wawe wamoja.


Lakini haya yote watawatenda kwa sababu ya jina langu, kwa kuwa hawamjui aliyenipeleka.


Na hayo watawatendeni kwa sababu hawakumjua Baba wala mimi.


Baba mwenye haki, ulimwengu haukukujua, lakini mimi nalikujua; na hawa walijua ya kuwa ndiwe uliyenituma.


Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hatta akampeleka Mwana wake wa pekee, illi mtu aliye yote amwaminiye asipotee, bali apate uzima wa milele.


Bali Mungu aonyesha pendo lake kwetu, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi.


Kwa maana viumbe vyote pia vinatazamia kwa shauku nyingi siku ile watakayofunuliwa wanawa Mungu.


katika tumaini: kwa kuwa viumbe vyenyewe navyo vitawekwa huru na kutolewa katika utumwa wa uharibifu viingie uhuru wa utukufu wa watoto wa Mungu.


Yeye asiyemwachilia Mwana wake yeye, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukarimia na vitu vyote pamoja nae?


Nami nitawakaribisheni, Nitakuwa Baba kwenu, Na ninyi mtakuwa kwangu wana na binti, anena Bwana Mwenyiezi.


Maana ninyi nyote ni wana wa Mungu kwa njia ya imani katika Yesu Kristo.


Na kama ninyi ni wa Kristo, bassi, nimekuwa mzao wa Ibrahimu, na wrarithi kwa ahadi.


Kwa maana mlikufa, na uzima wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu.


Hivi watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Shetani. Mtu aliye yote asiyefanya haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake.


Wapenzi, sasa tu wana wti Mungu, wala haijadhihirika bado tutakidokuwa: lakini twajua ya kuwa akidhihiri, tutafanana nae; kwa maana tutamwona kama alivyo.


Hivi pendo limekamilishwa kwetu, tuwe na ujasiri katika siku ya hukumu; kwa kuwa, kama yeye alivyo, ndivyo tulivyo na sisi ulimwenguni humu.


Yeye ashindae atayarithi haya, nami nitakuwa Mungu wake, nae atakuwa Mwana wangu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo