Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

1 Yohana 2:7 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

7 Ndugu, siwaandikii amri mpya, illa amri ya zamani mliyokuwa nayo tangu mwanzo.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Wapenzi wangu, amri hii ninayowaandikieni si amri mpya; ni amri ileile ya zamani mliyokuwa nayo tangu mwanzo. Amri hiyo ya zamani ni ule ujumbe mliousikia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Wapenzi wangu, amri hii ninayowaandikieni si amri mpya; ni amri ileile ya zamani mliyokuwa nayo tangu mwanzo. Amri hiyo ya zamani ni ule ujumbe mliousikia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Wapenzi wangu, amri hii ninayowaandikieni si amri mpya; ni amri ileile ya zamani mliyokuwa nayo tangu mwanzo. Amri hiyo ya zamani ni ule ujumbe mliousikia.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Wapendwa, siwaandikii ninyi amri mpya bali ile ya zamani, ambayo mmekuwa nayo tangu mwanzo. Amri hii ya zamani ni lile neno mlilosikia.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Wapendwa, siwaandikii ninyi amri mpya bali ile ya zamani, ambayo mmekuwa nayo tangu mwanzo. Amri hii ya zamani ni lile neno mlilosikia.

Tazama sura Nakili

1 Yohana 2:7
22 Marejeleo ya Msalaba  

Mmesikia walivyoambiwa, Mpende jirani yako, na, Mchukie adui yako:

Amri mpya nawapeni, mpendane; kama vile nilivyowapenda ninyi, na ninyi mpendane vivyo hivyo.

Wakamshika, wakamchukua hatta Areopago, wakisema, Je, twaweza kujua maana ya elimu hii mpya inenwayo nawe?

Lakini, wapenzi, ijapokuwa twanena hayo, katika khabari zenu tumesadiki mambo yaliyo mazuri zaidi, na yaliyo na wokofu:

Bassi, na yakae ndani yenu maneno yale mliyoyasikia tangu mwanzo. Neno lile mlilolisikia tangu mwanzo likikaa ndani yenu, ninyi nanyi mtakaa ndani ya Mwana, na ndani ya Baba.

Maana hii ndiyo khabari tuliyosikia tangu mwanzo, tupendane sisi kwa sisi;

Wapenzi, sasa tu wana wti Mungu, wala haijadhihirika bado tutakidokuwa: lakini twajua ya kuwa akidhihiri, tutafanana nae; kwa maana tutamwona kama alivyo.

Wapenzi, mioyo yetu isipotuhukumu, tuna ujasiri kwa Mungu;

Na hii ndiyo amri yake, tuliamini jina la Mwana wake Yesu Kristo, na kupendana, kama alivyotupa amri.

WAPENZI, msiamini kiila rolio, bali zijaribuni roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uwongo wengi wametokea duniani.

Wapenzi, ikiwa Mungu alitupenda sisi hivi, imetupasa na sisi kupendana.

Na amri hii tumepewa nae, ya kwamba yeye ampendae Mungu, ampende na ndugu yake.

Wapenzi, tupendane: kwa kuwa pendo ni la Mungu, na killa apendae amezaliwa na Mungu, nae anamjua Mungu.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo