Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Yohana 2:27 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

27 Na ninyi, mafuta, yale mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu, nanyi hamna haja ya mtu kuwafundisha; lakini kama yale mafuta yanavyokufundisheni khabari za mambo yote, tena ni kweli wala si uwongo, na kama yalivyokufundisheni, mnakaa ndani yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

27 Lakini, kwa upande wenu nyinyi, Kristo aliwatia mafuta kwa Roho wake. Na kama Roho huyo akiendelea kukaa ndani yenu, hamhitaji kufundishwa na mtu yeyote. Maana yeye anawafundisheni kila kitu, na mafundisho yake ni ya kweli, si ya uongo. Basi, shikeni mafundisho ya huyo Roho na kubaki katika muungano na Kristo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

27 Lakini, kwa upande wenu nyinyi, Kristo aliwatia mafuta kwa Roho wake. Na kama Roho huyo akiendelea kukaa ndani yenu, hamhitaji kufundishwa na mtu yeyote. Maana yeye anawafundisheni kila kitu, na mafundisho yake ni ya kweli, si ya uongo. Basi, shikeni mafundisho ya huyo Roho na kubaki katika muungano na Kristo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

27 Lakini, kwa upande wenu nyinyi, Kristo aliwatia mafuta kwa Roho wake. Na kama Roho huyo akiendelea kukaa ndani yenu, hamhitaji kufundishwa na mtu yeyote. Maana yeye anawafundisheni kila kitu, na mafundisho yake ni ya kweli, si ya uongo. Basi, shikeni mafundisho ya huyo Roho na kubaki katika muungano na Kristo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

27 Bali ninyi, upako mlioupata kutoka kwake unadumu ndani yenu, wala ninyi hamna haja ya mtu yeyote kuwafundisha. Lakini kama vile upako wake unavyowafundisha kuhusu mambo yote nayo ni kweli wala si uongo, basi kama ulivyowafundisha kaeni ndani yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

27 Nanyi, upako mlioupata kutoka kwake unakaa ndani yenu, wala ninyi hamna haja ya mtu yeyote kuwafundisha. Lakini kama vile upako wake unavyowafundisha kuhusu mambo yote nayo ni kweli wala si uongo, basi kama ulivyowafundisha kaeni ndani yake.

Tazama sura Nakili




1 Yohana 2:27
28 Marejeleo ya Msalaba  

Akajibu, akawaambia, Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za ufalme wa mbinguni, bali wale hawakujaliwa.


Na mimi nitamwomba Baba, nae atawapa Mfariji mwingine, akaae nanyi hatta milele,


Roho ya kweli; ambae ulimwengu hauwezi kumkubali, kwa kuwa haumwoni wala haumjui: bali ninyi mnamjua; maana anakaa kwenu, nae atakuwa ndani yenu.


Lakini Mfariji, Roho Mtakatifu, ambae Baba atampeleka kwa jina langu, yeye atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.


Lakini ajapo yeye, Roho ya kweli, atawaongozeni katika yote iliyo kweli: kwa maana hatasema kwa shauri lake yeye, lakini yote atakayosikia, atayasema, na mambo yajayo atawapasha khabari yake.


walakini ye yote atakaekunywa maji yale nitakayompa mimi, hataona kiu milele, bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujika hatta uzima wa milele.


Imeandikwa katika manabii, Na wote watakuwa wamefundishwa na Mungu. Bassi killa aliyesikia na kujifunza kwa Baba, huja kwangu.


Na sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho itokayo kwa Mungu, tupate kuyajua tuliyokarimiwa na Mungu.


Nayo twayanena, si kwa maneno tuliyofundishwa na hekima ya binadamu, bali tuliyofimdishwa na Roho, tukiyalinganisha mamho ya rohoni na mambo va rohoni.


Bassi Yeye atufanyae imara pamoja na ninyi katika Kristo, na kututia mafuta, ni Mungu,


mkiwa mwalimsikia mkafundishwa katika yeye, kama ilivyo kweli katika Yesu;


Bassi kama mlivyompokea Kristo Yesu, Bwana, enendeni vivyo hivyo katika yeye,


Kwa sababu hiyo sisi nasi twamshukuru Mungu bila kukoma, kwa kuwa mlipopokea lile neno la ujumbe la Mungu mlilolisikia kwetu, mlilipokea si kama neno la kibinadamu; bali kama neno la Mungu; na ndivyo lilivyo kweli kweli, litendalo kazi ndani yenu ninyi mnaoamini.


Kwa khabari ya upendano, hamna haja niwaandikie: maana ninyi wenyewe mmefundishwa na Mungu kupendana.


kwa ajili ya huo naliwekwa niwe mkhubiri na mtume (nasema kweli katika Kristo, sisemi uwongo), mwalimu wa mataifa katika imani na kweli.


kwa kuwa mmezaliwa marra ya pili, si kwa mbegu iharibikayo, bali isiyoharibika, kwa neno la Mungu lenye uzima, na lidumulo hatta milele.


Na sasa, watoto wadogo, kaeni ndani yake, illi, atakapofunuliwa, tuwe na ujasiri, wala tusiaibishwe mbele zake katika kuja kwake.


Nae azishikae amri zake hukaa ndani yake, nae ndani yake. Na hivi tunajua ya kuwa anakaa ndani yetu, kwa Roho aliyotupa.


kwa ajili ya ile kweli ikaayo ndani yetu, nayo itakuwa pamoja nasi hatta milele.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo