Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Yohana 2:21 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

21 Sikuwaandikia ninyi, kwa sababu hamwijui kweli, bali kwa sababu mwaijua, tena kwamba hapana uwongo wo wote utokao katika kweli.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 Basi, nawaandikieni, si kwa kuwa hamwujui ukweli, bali kwa sababu mnaujua; na pia mnajua kwamba uongo wowote haupatikani katika ukweli.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 Basi, nawaandikieni, si kwa kuwa hamwujui ukweli, bali kwa sababu mnaujua; na pia mnajua kwamba uongo wowote haupatikani katika ukweli.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 Basi, nawaandikieni, si kwa kuwa hamwujui ukweli, bali kwa sababu mnaujua; na pia mnajua kwamba uongo wowote haupatikani katika ukweli.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 Siwaandikii kwa sababu hamuijui kweli, bali kwa sababu mnaijua, nanyi mnajua hakuna uongo unaotoka katika kweli.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 Siwaandikii kwa sababu hamuijui kweli, bali kwa sababu mnaijua, nanyi mnajua hakuna uongo utokao katika kweli.

Tazama sura Nakili




1 Yohana 2:21
9 Marejeleo ya Msalaba  

Bassi Pilato akamwambia, Wewe u mfalme bassi? Yesu akajibu, Wewe wanena ya kwamba mimi ni mfalme. Mimi nalizaliwa kwa ajili ya haya na kwa ajili ya haya nalikuja ulimwenguni, illi niishuhudie kweli. Killa aliye wa kweli hunisikia sauti yangu.


Ninyi wa baba yenu Shetani, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzifanya. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo, wala hakusimama katika kweli kwa kuwa kweli hamna ndani yake. Asemapo uwongo, husema yaliyo yake mwenyewe, kwa sababu yu mwongo, na baba ya huo.


Bassi killa mtu awe mwepesi wa kusikia, mzito wa kusema, mzito wa ghadhabu;


Kwa hiyo sitakosa kuwakumbusheni hayo siku zote, ijapokuwa mnayajua na kuthubutishwa katika kweli iliyowatikia.


Hivi tutafahamu ya kwamba tu wa kweli, na mbele zake tutatuliza mioyo yetu


Tena napenda kuwakumbusha, ijapo mmekwisha kujua haya yote, ya kwamba Bwana, baada ya kuwaokoa watu katika inchi ya Misri, aliwaharibu wasioamini.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo