Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Yohana 2:19 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

19 Walitoka kwetu, bali hawukuwa wa kwetu. Maana kama wangalikuwa wa kwetu, wangalikaa pamoja nasi. Lakini walitoka illi wafunuliwe kwamba si wote walio wa kwetu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Watu hao wametokea kati yetu lakini hawakuwa kweli wa kwetu na ndiyo maana walituacha; kama wangalikuwa wa kwetu, wangalibaki nasi. Lakini waliondoka, wakaenda zao, kusudi ionekane wazi kwamba hawakuwa kamwe wa kwetu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Watu hao wametokea kati yetu lakini hawakuwa kweli wa kwetu na ndiyo maana walituacha; kama wangalikuwa wa kwetu, wangalibaki nasi. Lakini waliondoka, wakaenda zao, kusudi ionekane wazi kwamba hawakuwa kamwe wa kwetu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Watu hao wametokea kati yetu lakini hawakuwa kweli wa kwetu na ndiyo maana walituacha; kama wangalikuwa wa kwetu, wangalibaki nasi. Lakini waliondoka, wakaenda zao, kusudi ionekane wazi kwamba hawakuwa kamwe wa kwetu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu hasa. Kwa maana kama wangekuwa wa kwetu, wangekaa pamoja nasi; lakini kutoka kwao kulionesha kwamba hakuna hata mmoja wao aliyekuwa wa kwetu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu hasa. Kwa maana kama wangelikuwa wa kwetu, wangelikaa pamoja nasi, lakini kutoka kwao kulionyesha kwamba hakuna hata mmoja wao aliyekuwa wa kwetu.

Tazama sura Nakili




1 Yohana 2:19
30 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana wataondoka Makristo ya uwongo, na manabii ya uwongo, nao watafanyiza ishara kubwa ua mataajabu; wapate kuwadanganya, kama yumkini, hatta wateule.


kwa maana wataondoka Makristo wa nwongo, na manabii wa uwongo, watatoa ishara na ajabu, wapate kuwadanganya, kama yumkini, hatta wale wateule.


Na wale juu ya mwamba ndio wale ambao, walisikiapo neno, hulipokea kwa furaha; na hawa hawana mizizi, huamini kwa kitambo, na wakati wa kujaribiwa hujitenga.


Kilia tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na killa lizaalo hulisafisha illi lizidi kuzaa.


walakini ye yote atakaekunywa maji yale nitakayompa mimi, hataona kiu milele, bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujika hatta uzima wa milele.


Kwa kuwa tumesikia ya kwamba watu waliotoka kwetu wamewasumbueni kwa maneno yao, wakipotosha roho zenu, wakisema, ya kuwa hamna buddi kutahiriwa na kuishika Torati, ambao sisi hatukuwapa agizo lo lote;


tena katika baadhi yenu wataondoka watu, wakisema mapotofu, wawavute wanafunzi kwenda nyuma yao.


Si kana kwamba neno la Mungu limetanguka; maana hawawi wote Waisraeli walio wa uzao wa Israeli.


kwa maana lazima kuwapo uzushi kwenu, illi waliokubaliwa wawe dhahiri kwenu.


Kwa ajili ya hilo nastahimili yote, kwa ajili ya wateule, wao nao waupate wokofu ulio katika Kristo Yesu pamoja ua utukufu wa milele.


Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, wenye muhuri hii, Bwana awajua walio wake; tena, killa alilajae jina la Bwana na aache uovu.


Lakini hawataendelea sana; maana upumbavu wao utakuwa dhahiri kwa watu wote kama na wa hao ulivyokuwa.


Lakini sisi hatumo miongoni mwao wasitao na kupotea, bali miongoni mwao walio na imani ya kutuokoa roho zetu.


Kwa maana wadanganyifu wengi wameingia katika dunia, wasio-ungama ya kuwa Yesu Kristo yuaja katika mwili. Huyo ndiye yule mdanganyifu na adui wa Kristo.


YUDA, mtumwa wa Yesu Kristo, ndugu wa Yakobo, kwao waliopendwa katika Mungu Baba, na kuhifadhiwa kwa ajili ya Yesu Kristo baada ya kuitwa;


Watu hawo ndio wajitengao, watu wa dunia hii tu, wasio na Roho.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo