Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Yohana 2:18 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

18 Watoto, ni wakati wa mwisho: na kama vile mlivyosikia kwamba adui wa Kristo yuaja, hatta sasa adui wengi wa Kristo wamekwisha kuwapo. Kwa sababu hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Watoto, mwisho u karibu! Mlikwisha sikia kwamba mpinzani wa Kristo anakuja, na sasa wapinzani wengi wa Kristo wamekwisha fika, na hivyo twajua kwamba mwisho u karibu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 Watoto, mwisho u karibu! Mlikwisha sikia kwamba mpinzani wa Kristo anakuja, na sasa wapinzani wengi wa Kristo wamekwisha fika, na hivyo twajua kwamba mwisho u karibu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Watoto, mwisho u karibu! Mlikwisha sikia kwamba mpinzani wa Kristo anakuja, na sasa wapinzani wengi wa Kristo wamekwisha fika, na hivyo twajua kwamba mwisho u karibu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Watoto wadogo, huu ni wakati wa mwisho! Kama mlivyosikia kwamba anayempinga Al-Masihi anakuja, hivyo basi wanaompinga Al-Masihi wengi wamekwisha kuja. Kutokana na hili twajua kwamba huu ni wakati wa mwisho.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Watoto wadogo, huu ni wakati wa mwisho! Kama mlivyosikia kwamba anayempinga Al-Masihi anakuja, hivyo basi wanaompinga Al-Masihi wengi wamekwisha kuja. Kutokana na hili twajua kwamba huu ni wakati wa mwisho.

Tazama sura Nakili




1 Yohana 2:18
24 Marejeleo ya Msalaba  

Na manabii wengi wa uwongo wataondoka, watadanganya wengi.


Kwa maana wataondoka Makristo ya uwongo, na manabii ya uwongo, nao watafanyiza ishara kubwa ua mataajabu; wapate kuwadanganya, kama yumkini, hatta wateule.


Kwa maana wengi watakuja kwa jina langu, wakinena, Mimi ni Kristo; na watadanganya wengi.


Mimi ndiye: na watadanganya wengi.


Bassi Yesu akawaambia, Wanangu, mna kitoweo? Wakamjibu, Hapana.


Na hayo, tukiujua wakati, kwamba saa ya kuamka katika usingizi imekwisha kuwadia: kwa maana sasa wokofu u karibu yetu kuliko tulipoamini.


Usiku unakwisha, mchana umekaribia; bassi tuyavue matendo ya giza, tuzivae silaha za nuru.


mwisho wa siku bizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi yote, kwa yeye aliufanya ulimwengu.


aliyejuliwa tangu zamani, kabla haijawekwa misingi ya dunia; lakini alifimuliwa mwisho wa zamani kwa ajili yenu,


mnaolindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani mpate wokofu ulio tayari kufunuliwa wakati wa mwisho.


Mwisho wa mamho yote umekaribia; bassi, mwe na akili, mkakeshe katika sala:


LAKINI kuliondoka manabii wa uwongo katika watu, kama vile kwenu kutakavyokuwa waalimu wa uwongo, watakaoingiza kwa werevu uzushi wa kupoteza, wakimkana hatta Bwana aliyewanunua, wakijiletea uharibifu nsiokawia.


Mkijua kwanza neno hili ya kwamba katika siku za mwisho watakuja watu wenye kudhihaki, wafuatao tamaa zao wenyewe,


Naui aliye mwongo illa yeye akanae ya kuwa Yesu ni Kristo? Huyo ndiye adui wa Kristo, amkanae Baba na Mwana.


WAPENZI, msiamini kiila rolio, bali zijaribuni roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uwongo wengi wametokea duniani.


Na killa roho isiyoungama kwamba Yesu Kristo amekujii katika mwili, haitokani na Mungu. Na hii ndiyo roho ya adui wa Kristo ambae mmesikia kwamba yuaja; na sasa amekwisha kuwamo duniani.


Kwa maana wadanganyifu wengi wameingia katika dunia, wasio-ungama ya kuwa Yesu Kristo yuaja katika mwili. Huyo ndiye yule mdanganyifu na adui wa Kristo.


ya kwamba waliwaambia ya kuwa wakati wa mwisho watakuwuko watu wenye kudhihaki, wakizifuata tamaa zao wenyewe zilizo kinyume cha mapenzi ya Mungu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo