Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Yohana 2:17 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

17 Na dunia inapita, na tamaa yake, bali yeye afanyae mapenzi ya Mungu adumu hatta milele.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Ulimwengu pamoja na vitu vyake vyote vyenye kutamanika unapita; lakini mtu atendaye atakalo Mungu, anaishi milele.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Ulimwengu pamoja na vitu vyake vyote vyenye kutamanika unapita; lakini mtu atendaye atakalo Mungu, anaishi milele.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Ulimwengu pamoja na vitu vyake vyote vyenye kutamanika unapita; lakini mtu atendaye atakalo Mungu, anaishi milele.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Nao ulimwengu unapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu milele.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Nao ulimwengu unapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu milele.

Tazama sura Nakili




1 Yohana 2:17
28 Marejeleo ya Msalaba  

Katika hawa wawili ni yupi aliyefanya mapenzi ya baba yake? Wakamwambia, Yule wa kwanza. Yesu akawaambia, Amin, nawaambieni, watoza ushuru na makahaba wanatangulia mbele yenu kuingia katika ufalme wa Mungu.


Mbingu na inchi zitapita; bali maneno yangu hayatapita kamwe.


Siye killa mtu aniambiae, Bwana, Bwana, atakaeingia katika ufalme wa mbinguni; hali yeye afanyae mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.


Kwa maana mtu ye yote atakaeyafanya mapenzi ya Mungu, huyu ndive ndugu yangu, na umbu langu, na mama yangu.


walakini ye yote atakaekunywa maji yale nitakayompa mimi, hataona kiu milele, bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujika hatta uzima wa milele.


Huu ni mkale ulioshuka kutoka mbinguni; si kama baba zenu walivyoila manna wakafa; aulae mkate huu ataishi milele.


Mtu akipenda kuyatenda mapenzi yake, atajua khabari ya elimu hii kwamba yatoka kwa Mungu, au kwamba mimi nanena kwa nafsi yangu tu.


Wala msifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufunya upya nia zenu, mpate kujua kwa hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.


Na wale wautumiao ulimwengu huu, kama hawautumii sana; kwa maana mambo ya ulimwengu huu yanapita.


Kwa sababu hiyo na sisi, tangu siku tuliposikia, hatuachi kuwaombeeni, na kuomba dua, mjazwe maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa rohoni;


Epafra, aliye mtu wa kwenu, mtumwa wa Yesu Kristo, awasalimu, akifanya bidii siku zote kwa ajili yenu, katika maombi yake msimame wakamilifu mkathuhutike sana katika mapenzi yote ya Mungu.


Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na nasharati;


shukuruni kwa killa jambo; maana haya ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.


Maana mnahitaji uvumilivu, illi mkiisha kuyafanya mapenzi ya Mungu muipate abadi.


Uzima wenu ni nini? Maana ninyi moshi uonekanao kwa kitambo, kiisha hutoweka.


mnaolindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani mpate wokofu ulio tayari kufunuliwa wakati wa mwisho.


kuanzia sasa tusiendelee kuishi katika tamaa za wana Adamu, bali katika mapenzi ya Mungu, wakati wetu wa kukaa hapa duniani uliobakia.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo