Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Yohana 2:15 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

15 Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Msiupende ulimwengu, wala chochote kilicho cha ulimwengu. Mtu anayeupenda ulimwengu, upendo wa Baba hauwezi kuwamo ndani yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Msiupende ulimwengu, wala chochote kilicho cha ulimwengu. Mtu anayeupenda ulimwengu, upendo wa Baba hauwezi kuwamo ndani yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Msiupende ulimwengu, wala chochote kilicho cha ulimwengu. Mtu anayeupenda ulimwengu, upendo wa Baba hauwezi kuwamo ndani yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Msiupende ulimwengu wala mambo yaliyo ulimwenguni. Mtu yeyote akiupenda ulimwengu, upendo wa Baba haumo ndani yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Msiupende ulimwengu wala mambo yaliyo ulimwenguni. Kama mtu yeyote akiupenda ulimwengu, upendo wa Baba haumo ndani yake.

Tazama sura Nakili




1 Yohana 2:15
15 Marejeleo ya Msalaba  

Tena Shetani akamchukua hatta mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fakhari yake, akamwambia,


Hakuna mtu awezae kuwatumikia bwana wawili; kwa maana atamchukia mmoja, na kumpenda wa pili; au atamshika mmoja, na kumtweza wa pili. Hamwezi kumtumikia Mungu na mamona.


Hakuna mtumishi awezae kuwatumikia bwana wawili: maana au atamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na Mamona.


Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungeyapenda yaliyo yake: lakini kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu, bali mimi naliwachagua ninyi katika ulimwengu, kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia.


Wala msifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufunya upya nia zenu, mpate kujua kwa hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.


Maana sasa je! nawashawishi wana Adamu au Mungu? au nataka kuwapendeza wana Adamu? Kama ningekuwa hatta sasa nawapendeza wana Adamu, singekuwa mtumwa wa Kristo.


mlizoziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendae kazi sasa katika wana wa kuasi;


Maana shina moja la mabaya yote ni kupenda fedha, ambayo wengine wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani na kujichoma kwa maumivu mengi.


Dini iliyo safi na isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika shidda yao, na kujilinda pasipo mawaa katika dunia.


Enyi wazinzi, wanaume na wanawake, hamjui ya kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? bassi killa atakae kuwa rafiki wa dunia ajifanya kuwa adui wa Mungu.


Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia hii, akamwona ndugu yake yu muhitaji, akamzuilia huruma zake, je! huko ndiko kumpenda Mungu?


Hawo ni wa dunia; kwa biyo wanena ya dunia, dunia ikawasikia.


Amwaminiye Mwana wa Mungu anao ushuhuda ndani yake. Asiyemwamini Mungu amemfanya kuwa mwongo, kwa kuwa hakuuamini ushuhuda ambao Mungu amemsbuhudia Mwana wake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo