Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Yohana 1:9 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

9 Tukiziungama dhambi zetu, yu amini na wa haki atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha udhalimu wote.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Lakini tukiziungama dhambi zetu, basi, Mungu ni mwaminifu na mwadilifu, naye atatusamehe dhambi zetu na kututakasa uovu wote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Lakini tukiziungama dhambi zetu, basi, Mungu ni mwaminifu na mwadilifu, naye atatusamehe dhambi zetu na kututakasa uovu wote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Lakini tukiziungama dhambi zetu, basi, Mungu ni mwaminifu na mwadilifu, naye atatusamehe dhambi zetu na kututakasa uovu wote.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki, atatusamehe dhambi zetu na kutusafisha kutokana na udhalimu wote.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Kama tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki, atatusamehe dhambi zetu na kutusafisha kutoka kwenye udhalimu wote.

Tazama sura Nakili




1 Yohana 1:9
37 Marejeleo ya Msalaba  

wakabatizwa nae mtoni Yordani, wakiziungama dhambi zao.


Wakamwendea inchi yote ya Yahudi, nao wa Yerusalemi, wakabatizwa nae katika mto Yardani, wakiziungama dhambi zao.


Akakana, akisema, Mwanamke, simjui.


Baba mwenye haki, ulimwengu haukukujua, lakini mimi nalikujua; na hawa walijua ya kuwa ndiwe uliyenituma.


Na wengi wa wale walioamini wakaja wakaungama, wakidhihirisha matendo yao.


illi aonyeshe haki yake wakati huu, awe mwenye baki na mwenye kumpa haki yeye aaminiye kwa Yesu.


Mungu ni mwaminifu, ambae mliitwa nae muingie katika ushirika wa Mwana wake, Yesu Kristo Bwana wetu.


Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hizi; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa kuwa na haki katika jina la Bwana Yesu na katika Roho ya Mungu wetu.


kusudi alitakase na kulisafisha kwa maji, na kwa Neno;


Ni neno la kuaminiwa, listahililo kukubaliwa na watu wote, ya kwamba Kristo Yesu alikuja ulimwenguni, awaokoe wenye dhambi; na mimi wa kwanza wao.


aliyejitoa nafsi yake kwa ajili yetu, illi atuokoe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake, walio na juhudi kwa matendo mema.


Tulishike sana ungamo la tumaini letu, lisigeuke; maana yeye aliyeahidi ni amini;


Kwa imani hatta Sara mwenyewe alipokea nwezo wa kuwa na mimba, alipokuwa amepita wakati wake; kwa kuwa alimwona yeye aliyeahidi kuwa mwaminifu.


maana Mungu si dhalimu hatta asahau kazi zenu, na pendo lile mlilolidhihirisha kwa jina lake, kwa kuwa mmewakhudumia watakatifu, na hatta hivi sasa mngali mkiwakhudumia.


bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu Kristo, Mwana wake, yatusafisha dhambi zote.


Nao wauimba uimbo wa Musa, mtumishi wa Mungu, na uimbo wa Mwana kondoo, wakisema, Makuu, ya ajabu, matendo yako, ee Bwana Mungu Mwenyiezi; za haki, za kweli njia zako, ee Mfalme wa watakatifu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo