Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Yohana 1:8 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

8 Tukisema hatuna dhambi, twajidanganya, wala kweli haimo mwetu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Tukisema kwamba hatuna dhambi, tunajidanganya wenyewe, na ukweli haumo ndani yetu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Tukisema kwamba hatuna dhambi, tunajidanganya wenyewe, na ukweli haumo ndani yetu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Tukisema kwamba hatuna dhambi, tunajidanganya wenyewe, na ukweli haumo ndani yetu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe wala kweli haimo ndani yetu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Kama tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe wala kweli haimo ndani yetu.

Tazama sura Nakili




1 Yohana 1:8
33 Marejeleo ya Msalaba  

Ninyi wa baba yenu Shetani, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzifanya. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo, wala hakusimama katika kweli kwa kuwa kweli hamna ndani yake. Asemapo uwongo, husema yaliyo yake mwenyewe, kwa sababu yu mwongo, na baba ya huo.


kama ilivyoandikwa, ya kama, Hakuna mwenye haki hatta mmoja.


Maana hapana tofauti; kwa sababu wote wamefanya dhambi, wanaona kwamba wamepungukiwii utukufu wa Mungu:


Mtu asijidanganye nafsi yake: kama mtu akijiona kuwa mweuye hekima kati yeuu katika dunia hii, na awe mpumbavu, apate kuwa mwenye hekima.


Maana mtu akijiona kuwa kitu, nae si kitu, ajidanganya nafsi yake.


na majadiliano ya watu walioharibiwa akili zao, walioikosa kweli, wakidhani ya kuwa utawa ni njia ya kupata faida; ujitenge na watu kama hao,


Lakini watu wabaya na wadanganyaji wataendelea na kuzidi kuwa waovu, wakidanganya na wakidanganyika.


Mwe watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, mkijidanganya nafsi zenu.


Mtu akidhani ya kuwa ana dini, nae hazuii ulimi wake kwa khatamu, akijidanganya moyo wake, dini yake mtu yule haifai.


Maana twajikwaa sisi sote pia katika mambo mengi. Mtu asiyejikwaa katika kunena, huyo ni mtu mkamilifu, awezae kuuzuia na mwili wake wote kama kwa lijamu.


wakipatwa na madhara, ujira wa udhalimu wao, wakidhani kuwa ulevi wakati wa mchana ni anasa; ni mawaa na aibu, wakifuata anasa katika karamu zao za upendo, wafanyapo karamu pamoja nanyi;


Tukisema hatukutenda dhambi, twamfanya mwongo wala neno lake halimo mwetu.


Tukisema twashirikiana nae, tena tukienenda gizani, twasema uwongo, wala hatuifanyi iliyo kweli;


Yeye asemae, Nimemjua, nae hazishiki amri zake, ni mwongo, na kweli haimo ndani yake.


Mtu akisema, Nampenda Mungu, nae anamchukia ndugu yake, yu mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambae amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambae hakumwona.


kwa ajili ya ile kweli ikaayo ndani yetu, nayo itakuwa pamoja nasi hatta milele.


Maana nalifurahi mno walipokuja ndugu na kuishuhudia kweli yako, kama nendavyo katika kweli.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo