Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Yohana 1:6 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

6 Tukisema twashirikiana nae, tena tukienenda gizani, twasema uwongo, wala hatuifanyi iliyo kweli;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Tukisema kwamba tuna umoja naye, na papo hapo tunaishi gizani, tutakuwa tumesema uongo wala hatuishi kwa ukweli kwa maneno na matendo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Tukisema kwamba tuna umoja naye, na papo hapo tunaishi gizani, tutakuwa tumesema uongo wala hatuishi kwa ukweli kwa maneno na matendo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Tukisema kwamba tuna umoja naye, na papo hapo tunaishi gizani, tutakuwa tumesema uongo wala hatuishi kwa ukweli kwa maneno na matendo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Tukisema kwamba twashirikiana naye huku tukienenda gizani, twasema uongo, wala hatutendi lililo kweli.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Kama tukisema kwamba twashirikiana naye huku tukienenda gizani, twasema uongo, wala hatutendi lililo kweli.

Tazama sura Nakili




1 Yohana 1:6
25 Marejeleo ya Msalaba  

Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kufukuza pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?


Bali akienda usiku, hujikwaa, kwa sababu nuru haimo ndani yake.


Bassi Yesu akawaambia, Nuru ingali pamoja nanyi muda kitambo. Enendeni maadam mnayo ile nuru, giza lisije likawaweza; nae aendae gizani hajui aendako.


Mimi nimekuja niwe nuru ulimwenguni, illi kilia aniaminiye mimi asikae gizani.


Bassi Yesu akanena nao tena, akisema. Mimi ni nuru ya ulimwengu; anifuatae hatakwenda katika giza kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.


Nanyi hamkumjua; lakini mimi namjua, na nikisema ya kwamba simjui, nitakuwa mwongo kama ninyi; lakini namjua na neno lake nalishika.


kwa unafiki wa watu wasemao uwongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe;


Yafaa nini, ndugu zangu, mtu akisema ana imani, nae hana matendo? Je! ile imani yaweza kumwokoa?


mtu wa kwenu akawaambia, Enendeni zenu kwa amani, mkaote moto na kushiba, illakini asiwape mahitaji ya mwili, yafaa nini?


Lakini mtu atasema, Wewe una imani, nami nina matendo. Nionyeshe imani yako pasipo matendo yako, nami nitakuonyesha imani yangu kwa matendo yangu.


Tukisema hatukutenda dhambi, twamfanya mwongo wala neno lake halimo mwetu.


tuliyoiona na kuisikia, twawakhubiri ninyi; ninyi nanyi mpate kushirikiana na sisi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo.


Tukisema hatuna dhambi, twajidanganya, wala kweli haimo mwetu.


Yeye asemae, Nimemjua, nae hazishiki amri zake, ni mwongo, na kweli haimo ndani yake.


Mtu akisema, Nampenda Mungu, nae anamchukia ndugu yake, yu mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambae amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambae hakumwona.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo