Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Yohana 1:5 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

5 Na hii ndiyo khabari tuliyoisikia kwake, na kuikhubiri kwenu, ya kwamba Mungu ni nuru, wala giza yo yote hamna ndani yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Basi, habari tuliyoisikia kwake Yesu na tunayowahubirieni ndiyo hii: Mungu ni mwanga na hamna giza lolote ndani yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Basi, habari tuliyoisikia kwake Yesu na tunayowahubirieni ndiyo hii: Mungu ni mwanga na hamna giza lolote ndani yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Basi, habari tuliyoisikia kwake Yesu na tunayowahubirieni ndiyo hii: Mungu ni mwanga na hamna giza lolote ndani yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Huu ndio ujumbe tuliosikia kutoka kwake na kuwatangazia ninyi: kwamba Mungu ni nuru na ndani yake hamna giza lolote.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Huu ndio ujumbe tuliosikia kutoka kwake na kuwatangazia ninyi: kwamba Mungu ni nuru na ndani yake hamna giza lolote.

Tazama sura Nakili




1 Yohana 1:5
19 Marejeleo ya Msalaba  

Na huu ndio ushuhuda wake Yohana, Wayahudi walipotuma makuhani na Walawi toka Yerusalemi wamwulize, Wewe u nani?


Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao uzima ulikuwa nuru ya watu,


Kulikuwako nuru halisi, imtiayo nuru killa mtu ajae katika ulimwengu.


Bassi Yesu akanena nao tena, akisema. Mimi ni nuru ya ulimwengu; anifuatae hatakwenda katika giza kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.


Maadam nipo ulimwenguni, mimi ni nuru ya ulimwengu.


Kwa maana mimi nalipokea kwa Bwana niliyowakhubirini, ya kuwa Bwana Yesu usiku ule aliotolewa alitwaa mkate,


ambae yeye peke yake hapatikani na mauti, akaae katika nuru isiyoweza kukaribiwa; wala hapana mwana Adamu aliyemwona, wala awezae kumwona, ndiye mwenye heshima na uweza milele. Amin.


Killa kutoa kwenia, na killa kitolewacho kilicho kamili, chatoka juu, chashuka kwa Baba wa mianga, kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeukageuka.


Maana hii ndiyo khabari tuliyosikia tangu mwanzo, tupendane sisi kwa sisi;


Na mji ule hauhitaji jua wala mwezi uuangaze, kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru, na taa yake ni Mwana kondoo.


Wala hapatakuwa usiku huko; wala hawana haja ya taa wala ya nuru ya jua; kwa kuwa Bwana Mungu awatia nuru, nao watamiliki milele hatta milele.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo