Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Yohana 1:1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 ILIYOKUWA tangu mwanzo, tuliyoisikia, tuliyoiona kwa macho yetu, tuliyoitazama, na mikono yetu ikaipapasa, kwa khabari ya Neno la uzima,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Habari hii yahusu Neno la uhai lililokuwako tangu mwanzo. Sisi tumepata kulisikia na kuliona kwa macho yetu wenyewe; tulilitazama na kulishika kwa mikono yetu wenyewe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Habari hii yahusu Neno la uhai lililokuwako tangu mwanzo. Sisi tumepata kulisikia na kuliona kwa macho yetu wenyewe; tulilitazama na kulishika kwa mikono yetu wenyewe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Habari hii yahusu Neno la uhai lililokuwako tangu mwanzo. Sisi tumepata kulisikia na kuliona kwa macho yetu wenyewe; tulilitazama na kulishika kwa mikono yetu wenyewe.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Tunawajulisha lile lililokuwako tangu mwanzo, lile tulilosikia, ambalo tumeliona kwa macho yetu, ambalo tumelitazama na kuligusa kwa mikono yetu, kuhusu Neno la uzima.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Tunawajulisha lile lililokuwepo tangu mwanzo, lile tulilosikia, ambalo tumeliona kwa macho yetu, ambalo tumelitazama na kuligusa kwa mikono yetu, kuhusu Neno la uzima.

Tazama sura Nakili




1 Yohana 1:1
23 Marejeleo ya Msalaba  

kama walivyotuhadithia wale waliokuwa mashahidi, ua watumishi wa lile neno tokea mwanzo,


Tazameni mikono yangu, na miguu yangu, ya kuwa ni mimi mwenyewe. Nipapaseni, mkatazame; kwa maana pepo hana mwili na mifupa, kama mnionavyo mimi kuwa nayo.


Nae aliyeona ameshuhudu, na ushuhuda wake ni kweli; na yeye anajua ya kuwa asema kweli, ninyi mpate kuamini.


Akiisha akamwambia Tomaso, Lete hapa kidole chako, ukatazame mikono yangu; kalete mkono wako, uutie katika ubavu wangu; wala nsiwe asiyeamini, bali aaminiye.


Maana kama vile Baba alivyo na uzima nafsini mwake, vivyo hivyo alimpa na Mwana kuwa na uzima nafsini mwake;


Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Kabla Ibrahimu hajakuwapo, Mimi nipo.


na baada ya kuteswa kwake, akawadhihirisbia ya kwamba yu hayi, kwa dalili nyingi, akiwatokea muda wa siku arubaini, na kuyanena mambo yaliyonkhusu ufalme wa Mungu.


Kwamba ni haki mbele za Mungu kuwasikiliza ninyi kuliko Mungu, hukumuni ninyi wenyewe; maana sisi hatuwezi kuacha kuyanena mambo tuliyoyaona na kuyasikia.


sisi je! tutapataje kujiponya, tusipotunza wokofu mkiju namna hii? ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kiisha nkathubutika kwetu na wale waliosikia;


Na sisi tumeona na kushuhudu ya kuwa Baba amempeleka Mwana kuwa Mwokozi wa ulimwengu.


Kwa maana watatu ni mashahidi mbinguni, Baba, Neno, na Robo Mtakatifu, ua watatu hawa ni umoja.


ikinena, Mimi ni Alfa na Omega, wa kwanza na wa mwisho. Haya uonayo yaandike katika chuo, ukayapeleke kwa makanisa saba yaliyo katika Asia; Efeso, na Smurna, na Pergamo, na Thuatera, na Sardi, na Filadelfia, na Laodikia.


Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisiio, asema Bwana Mungu, alioko, aliyekuwako, na atakaekuwako, Mwenyiezi.


Nae amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na, jina lake, aitwa, Neno la Mungu.


Na kwa malaika wa kanisa lililo katika Smurna andika; Haya ayanena yeye aliye wa kwanza na wa mwisbo, aliyekuwa amekufa, akawa hayi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo