Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wathesalonike 5:21 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

21 jaribuni vyote; lishikeni lililo jema;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 Pimeni kila kitu: Zingatieni kilicho chema,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 Pimeni kila kitu: Zingatieni kilicho chema,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 Pimeni kila kitu: zingatieni kilicho chema,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 Jaribuni kila kitu. Yashikeni yaliyo mema.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 Jaribuni kila kitu. Yashikeni yaliyo mema.

Tazama sura Nakili




1 Wathesalonike 5:21
40 Marejeleo ya Msalaba  

Na mbona ninyi katika nafsi zenu hamwamui yaliyo haki?


Kaeni ndani yangu, na mimi ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu, kadhalika na ninyi, msipokaa ndani yangu.


Bassi Yesu akawaamhia Wayahudi wale waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mu wanafunzi wangu kweli kweli;


Nae, alipokwisha kufika na kuiona neema ya Mungu akafurahi, akawasihi wote waambatane na Bwana kwa kusudi la moyo.


wakifanya imara roho za wanafunzi na kuwaonya wakae katika imani, na ya kwamba imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya shidda nyingi.


Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa Thessaloniki, kwa kuwa walilipokea Neno kwa uelekefu wa moyo, wakayachunguza maandiko, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo.


Wala msifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufunya upya nia zenu, mpate kujua kwa hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.


Pendo niwe nalo pasipo unafiki; mkichukia lililo ovu, mkiambatana na lililo jema.


Bassi, ndugu wapendwa, mwe imara, msiotikisika, mkizidi sana kutenda kazi ya Bwana siku zote, kwa kuwa taabu yenu siyo burre katika Bwana.


Maana ni nani ayajuae mambo ya bin Adamu illa roho ya bin Adamu iliyo ndani yake? Na vivyo hivyo mambo ya Mungu hakuna ayajuae illa Roho ya Mungu.


Tuwapo na nafasi na tuwatendee watu wote mema; khassa watu walio wa nyumba ya imani.


mkihakiki nini impendezayo Bwana.


mpate kuyakubali yaliyo mema; illi mwe na mioyo safi, bila kosa, mpaka siku ya Kristo,


Illakini, hapo tulipofika na tuenende kwa kanuni ile ile.


Khatimae, ndugu zangu, mambo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya heshima, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye kuvuma vizuri, ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini haya.


Angalieni mtu awae yote asimlipe mwenziwe mabaya kwa mabaya; bali siku zote lifuateni lililo jema, ninyi kwa ninyi na kwa watu wote.


jitengeni na ubaya wa killa namna.


Bassi, ndugu, simameni imara, mkayashike mapokeo mliyofundishwa, ikiwa kwa maneno, au kwa waraka wetu.


Wajua hili, ya kuwa wote walio katika Asia wameniacha, katika hao ni Figello na Hermogene.


Kwa maana katika hawa wamo wale wajiingizao kalika nyumba za watu, na kuchukua mateka wanawake wajinga wenye mizigo ya dhambi, waliochukuliwa na tamaa za namna nyingi,


Iskander mfua shaba alinionya mabaya mengi; Bwana atamlipa kwa jinsi ya matendo yake.


Tulishike sana ungamo la tumaini letu, lisigeuke; maana yeye aliyeahidi ni amini;


WAPENZI, msiamini kiila rolio, bali zijaribuni roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uwongo wengi wametokea duniani.


Najua matendo yako, na taabu yako, na uvumilivu wako, na ya kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wajiitao mitume, nao sio, ukawaona kuwa wawongo;


Illa mlicho nacho kishikeni, hatta nitakapokuja.


Tazama, naja upesi. Shika sana ulicho nacho asije mtu akaitwaa taji yako.


Bassi kumbuka jinsi ulivyopokea, na jinsi ulivyosikia; yashike hayo na kutubu. Illakini usipokesha nitakuja kwako kama mwizi, nawe hutaijua saa nitakayokuja kwako.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo