Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wathesalonike 5:15 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

15 Angalieni mtu awae yote asimlipe mwenziwe mabaya kwa mabaya; bali siku zote lifuateni lililo jema, ninyi kwa ninyi na kwa watu wote.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Angalieni mtu yeyote asimlipe mwingine maovu kwa maovu, ila nia yenu iwe kutendeana mema daima na kuwatendea mema watu wote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Angalieni mtu yeyote asimlipe mwingine maovu kwa maovu, ila nia yenu iwe kutendeana mema daima na kuwatendea mema watu wote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Angalieni mtu yeyote asimlipe mwingine maovu kwa maovu, ila nia yenu iwe kutendeana mema daima na kuwatendea mema watu wote.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Angalieni kuwa mtu asimlipe mwenzake maovu kwa maovu, bali siku zote tafuteni kutendeana mema ninyi kwa ninyi na kwa watu wote.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Angalieni kuwa mtu asimlipe mwenzake maovu kwa maovu, bali siku zote tafuteni kutendeana mema ninyi kwa ninyi na kwa watu wote.

Tazama sura Nakili




1 Wathesalonike 5:15
39 Marejeleo ya Msalaba  

bali mimi nawaambieni, Msishindane na mtu mwovu; bali mtu akupigae shavu la kuume, mgeuzie na la pili.


Bali wapendeni adui zenu, katendeni kwa ihsani, kopeshani, bali kutumaini kupata kitu tena: na thawabu yenu itakuwa nyingi, na mtakuwa wana wa Aliye juu sana; kwa sabahu Yeye yu mwema kwa watu wasio na shukrani, na waovu.


Paolo akapaaza sauti yake kwa uguvu, akisema, Usijidhuru, kwa maana sisi sote tupo hapa.


Pendo niwe nalo pasipo unafiki; mkichukia lililo ovu, mkiambatana na lililo jema.


Bassi kama ni hivyo, tufuate mambo ya amani na mambo yafaayo kwa kujengana.


UFUATIENI upendo, katakeni sana karama za rohoni, lakini zaidi mpate kukhutubu.


Lakini, Timotheo akija, angalieni akae kwenu pasipo khofu; maana anaifanya kazi ya Bwana kama mimi nami:


Bassi imekuwa upungufu kwenu kabisa kwamba mnashitakiana ninyi kwa ninyi. Maana si afadhali kudhulumiwa? Maana si afadhali kunyangʼanywa mali zenu?


Tuwapo na nafasi na tuwatendee watu wote mema; khassa watu walio wa nyumba ya imani.


Angalieni sana, bassi, jinsi mnavyoenenda, si kama watu wasio hekima, bali kama wenye hekima;


Illakini killa mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe; na mke asikose kumstahi mumewe.


illi mwenende kama ilivyo wajib wenu kwa Mungu mwenende, awaitae muingie katika ufalme wake na utukufu wake.


jaribuni vyote; lishikeni lililo jema;


Bali wewe, mtu wa Mungu, yakimbie hayo, ukafuate haki, utawa, imani, upendo, uvumilivu, upole.


Tena haimpasi mtumwa wa Bwana kuwa mgomvi, bali kuwa mwanana kwa watu wote, awezae kufundisha, mvumilivu,


wasimtukane mtu, wasiwe wagomvi, wawe wema, wakionyesha upole wote kwa watu wote.


Fanyeni bidii kutafuta amani kwa watu wote, na utakatifu, ambao hapana mtu atakaemwona Mungu asipokuwa nao;


Mkiisha kujisafisha roho zenu kwa kuitii kweli, kwa Roho, kiasi cha kuufikilia upendano usio na unafiki, bassi jitahidini kupendana kwa moyo;


Heshimuni walu wote. Upendeni udugu. Mcheni Mungu. Mpeni heshima mfalme.


watu wasiolipa baya badala ya baya, au laumu badala ya laumu; bali wabarikio; kwa sababu ndiyo mlioitiwa illi mrithi baraka.


Mpenzi, usiuige ubaya, bali wema. Yeye atendae mema ni wa Mungu, bali yeye atendae mabaya hakumwona Mungu.


Nikaanguka mbele ya miguu yake, nimsujudie, akaniambia, Angalia, usifanye hivi: mimi mjoli wako na mmoja wa ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Msujudu Mungu: kwa maana ushuhuda wa Yesu ni roho ya unabii.


Akaniambia, Angalia, usifanye hivyo; mimi mjoli wako, na wa ndugu zako manabii na wa wale washikao maneno ya kitabu hiki. Msujuduni Mungu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo