Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wathesalonike 5:14 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

14 Twawasihi, ndugu, waonyeni wale wasiokaa kwa taratihu, watieni moyo walio dhaifu, watieni nguvu wanyonge, vumilieni na watu wote.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Ndugu, tunawahimizeni muwaonye watu walio wavivu, muwatie moyo watu wanyonge, muwasaidie watu dhaifu, muwe na subira kwa wote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Ndugu, tunawahimizeni muwaonye watu walio wavivu, muwatie moyo watu wanyonge, muwasaidie watu dhaifu, muwe na subira kwa wote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Ndugu, tunawahimizeni muwaonye watu walio wavivu, muwatie moyo watu wanyonge, muwasaidie watu dhaifu, muwe na subira kwa wote.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Nasi twawasihi, ndugu, waonyeni walio wavivu, watieni moyo waoga, wasaidieni wanyonge na kuwavumilia watu wote.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Nasi twawasihi, ndugu, waonyeni walio wavivu, watieni moyo waoga, wasaidieni wanyonge na kuwavumilia watu wote.

Tazama sura Nakili




1 Wathesalonike 5:14
40 Marejeleo ya Msalaba  

Mwanzi uliopondeka hatauvunja, Wala kitani kitokacho moshi hatakizima, Hatta aletapo hukumu yake ikashinda.


lakini nimekuombea, illi imani yako isipunguke; nawe uongokapo, wathubutishe ndugu zako.


Kwa maana sikujiepusha na kuwakhubirini khabari ya shauri lote la Mungu.


Kwa biyo kesheni, mkikumbuka kama miaka mitatu, usiku na mchana, sikuacha kumwonya killa mtu kwa machozi.


Nimewapeni mfano katika mambo yote ya kuwa kwa kushika kazi hivi imewapaseni kuwasaidia wasio na nguvu, na kuyakumbuka maneno ya Bwana Yesu, jinsi alivyosema mwenyewe, Ni kheri kutoa kuliko kupokea.


BASSI, nawasihi, ndugu, kwa huruma zake Mungu, mtoe miili yenu iwe dhabihu hayi, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ibada yenu yenye maana.


LAKINI yeye aliye dhaifu wa imani, mkaribisheni, illakini msimhukumu mawazo yake.


Siyaandiki haya illi kuwatahayarisha, hali kuwaonya kama watoto niwapendao. Maana ijapokuwa mna waalimu elfu katika Kristo, illakini hamna baba wengi.


Bali elimu hii haimo ndani ya watu wote; illa wengine kwa kuizoelea ile sanamu hatta sasa hula kama ni kitu kilichotolewa sadaka kwa sanamu; na dhamiri yao, kwa kuwa dhaifu, hunajisika.


Lakini matunda ya Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,


kwa unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilivu, mkichukuliana katika upendano;


tena mwe wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkiachiliana, kama na Mungu katika Kristo alivyowaachilia ninyi.


ambae sisi tunakhubiri khabari zake, tukimwonya killa mtu, na tukimfundisha killa mtu katika hekima yote, tupate kumleta killa mtu mtimilifu katika Kristo Yesu;


illakini msimhesabu kuwa adui, bali mwonyeni kama ndugu.


si mtu wa kuzoelea mvinyo, si mpigaji, si mtu apendae fedha; bali awe mpole, asiwe mtu wa kujadiliana, asitamani fedha;


Bali wewe, mtu wa Mungu, yakimbie hayo, ukafuate haki, utawa, imani, upendo, uvumilivu, upole.


likhubiri neno, fanya bidii, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, kaonya kwa uvumilivu wote na mafundisho.


Maana wako wengi wasiotii, wenye maneno yasiyo maana, wadanganyaji, khassa wale waliotahiriwa,


ikiwa mtu hakushitakiwa neno, nae ni mume wa mke mmoja, ana watoto waaminio, wasioshitakiwa kuwa ni asharati na wasiotii.


Kwa hiyo inyosheni mikono iliyolegea na magoti yaliyopooza,


Wakumbukeni waliofungwa kana kwamba mmefungwa pamoja nao; nao wanaodhulumiwa, kwa kuwa nanyi m katika mwili.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo