Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wathesalonike 4:9 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

9 Kwa khabari ya upendano, hamna haja niwaandikie: maana ninyi wenyewe mmefundishwa na Mungu kupendana.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Hakuna haja ya kuwaandikieni juu ya kuwapenda ndugu zenu waumini. Nyinyi wenyewe mmefundishwa na Mungu namna mnavyopaswa kupendana.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Hakuna haja ya kuwaandikieni juu ya kuwapenda ndugu zenu waumini. Nyinyi wenyewe mmefundishwa na Mungu namna mnavyopaswa kupendana.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Hakuna haja ya kuwaandikieni juu ya kuwapenda ndugu zenu waumini. Nyinyi wenyewe mmefundishwa na Mungu namna mnavyopaswa kupendana.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Sasa kuhusu upendo wa ndugu hamna haja mtu yeyote kuwaandikia, kwa maana ninyi wenyewe mmefundishwa na Mungu kupendana.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Sasa kuhusu upendo wa ndugu hamna haja mtu yeyote kuwaandikia, kwa maana ninyi wenyewe mmefundishwa na Mwenyezi Mungu kupendana.

Tazama sura Nakili




1 Wathesalonike 4:9
30 Marejeleo ya Msalaba  

Na ya pili yafanana nayo, ndiyo hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako.


Lakini Mfariji, Roho Mtakatifu, ambae Baba atampeleka kwa jina langu, yeye atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.


Na jamii ya watu walioamini walikuwa moyo mmoja na roho moja: wala hapana mmoja aliyesema ya kuwa kitu cho chote alicho nacho ni mali yake mwenyewe; bali walikuwa na vitu vyote shirika.


Kwa pendo la udugu, mwe na shauku ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu;


KWA khabari za kuwakhudumia watakatifu sina haja ya kuwaandikia.


Bassi sisi tulio wakamilifu na tuwaze hayo; na hatta mkiwaza mengine katika lo lote, Mungu atawafunulieni hilo nalo.


LAKINI kwa khabari ya nyakati na majira, ndugu, hamna haja niwaandikie.


Hili ni agano nitakalowapa baada ya siku zile, anna Bwana, Nitatia sharia zangu mioyoni mwao, na katika akili zao nitaziandika; ndipo anenapo.


Neno la mwisbo ni hili; mwe na nia moja, wahurumianao, wenye kupendana kama ndugu, wasikitikivu, wanyenyekevu;


zaidi ya yote mwe na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husetiri wingi wa dhambi;


na katika utawa wenu upendano wa ndugu, na katika upendano wa ndugu, upendo.


Yeye ampendae ndugu yake, akaa katika nuru, wala ndani yake hamna kikwazo.


Maana hii ndiyo khabari tuliyosikia tangu mwanzo, tupendane sisi kwa sisi;


Na hii ndiyo amri yake, tuliamini jina la Mwana wake Yesu Kristo, na kupendana, kama alivyotupa amri.


Na amri hii tumepewa nae, ya kwamba yeye ampendae Mungu, ampende na ndugu yake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo