Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wathesalonike 4:4 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

4 killa mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Kila mwanamume anapaswa kujua namna ya kuishi na mkewe kwa utakatifu na heshima,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Kila mwanamume anapaswa kujua namna ya kuishi na mkewe kwa utakatifu na heshima,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Kila mwanamume anapaswa kujua namna ya kuishi na mkewe kwa utakatifu na heshima,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 na kila mmoja wenu ajifunze kuutawala mwili wake mwenyewe katika utakatifu na heshima,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 ili kwamba kila mmoja wenu ajifunze kuutawala mwili wake mwenyewe katika utakatifu na heshima,

Tazama sura Nakili




1 Wathesalonike 4:4
15 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini Bwana akamwambia, Shika njia; kwa maana huyu ni chombo kiteule kwangu, alichukue Jina langu mbele ya mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli.


Kwa ajili ya bayo Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, waufuate uchafu, hatta wakavunjiana heshima miili yao:


BASSI, nawasihi, ndugu, kwa huruma zake Mungu, mtoe miili yenu iwe dhabihu hayi, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ibada yenu yenye maana.


Nasema kwa jinsi ya kibinadamu kwa sababu ya udhaifu wa miili yenu. Kwa maana kama mlivyotoa viungo vyenu vitumiwe na uchafu na maasi mpate kuasi, vivyo sasa toeni viungo vyenu vitumiwe na haki mpate kutakaswa.


Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Bassi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaha? Hasha!


Lakini kwa sababu ya mambo ya zina killa mtu na awe na mke wake mwenyewe, na killa mwanamke na awe na mume wake mwenyewe.


Lakini kama hawawezi kujizuia, na waoe; maana ni afadhali kuoa kuliko kuwaka moto.


Lakini tuna hazina hii katika vyombo vya udongo, illi adhama ya uwezo iwe ya Mungu, wala si yetu sisi.


Khatimae, ndugu zangu, mambo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya heshima, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye kuvuma vizuri, ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini haya.


Ndoa iheshimiwe na watu wote, na malalo yawe safi: kwa maana waasharati na wazinzi Mungu atawahukumu.


Ninyi wanme kadhalika, kaeni na wake zenu kwa akili; mkimpa mke heshima, kama chombo kisieho nguvu, na kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudi sala zenu zisizuiliwe.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo