Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wathesalonike 4:16 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

16 Kwasababu Bwana mwenyewe atasbuka kutoka mbinguni na sauti kuu na sauti ya malaika mkuu, na panda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo, watafufuliwa kwanza;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Maana patatolewa amri, sauti ya malaika mkuu, sauti ya tarumbeta ya Mungu, naye Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni. Ndipo wale waliokufa wakiwa wanamwamini Kristo watafufuliwa kwanza.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Maana patatolewa amri, sauti ya malaika mkuu, sauti ya tarumbeta ya Mungu, naye Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni. Ndipo wale waliokufa wakiwa wanamwamini Kristo watafufuliwa kwanza.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Maana patatolewa amri, sauti ya malaika mkuu, sauti ya tarumbeta ya Mungu, naye Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni. Ndipo wale waliokufa wakiwa wanamwamini Kristo watafufuliwa kwanza.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Kwa maana Bwana Isa mwenyewe atashuka kutoka mbinguni, akitoa amri kwa sauti kuu, pamoja na sauti ya malaika mkuu, na sauti ya tarumbeta ya Mungu. Nao waliokufa wakiwa katika Al-Masihi watafufuka kwanza.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Kwa maana Bwana Isa mwenyewe atashuka kutoka mbinguni, akitoa amri kwa sauti kuu, pamoja na sauti ya malaika mkuu, na sauti ya tarumbeta ya Mungu. Nao waliokufa wakiwa katika Al-Masihi watafufuka kwanza.

Tazama sura Nakili




1 Wathesalonike 4:16
33 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atamlipa killa mtu kwa kadiri ya kutenda kwake.


Amin, nawaambieni, Pana watu katika hawo wanaosimama hapa, ambao hawataonja mauti kabisa, hatta watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika ufalme wake.


Hatta atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja nae, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake:


Yesu akamwambia. Wewe umesema: lakini nawaambieni, Tangu sasa mtamwoua Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kuume wa nguvu, akija juu ya mawingu.


wakasema, Watu wa Galilaya, mbona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi hiyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni.


Na hapo wao nao waliolala katika Kristo wamepotea.


Lakini sasa Kristo amefufuka, limbuko lao waliolala.


Lakini killa mmoja mahali pake; limbuko Kristo; baadae walio wake Kristo, atakapokuja.


na kumugojea Mwana wake kutoka mbinguni, ambae alimfufua katika wafu, Yesu, anaetuokoa na ghadhabu itakayokuja.


Bassi Mungu mwenyewe, Baba yetu, na Bwana wetu Yesu Kristo atuongoze njia yetu tufike kwenu;


na kuwalipa ninyi mteswao raha pamoja na sisi wakati wa kufunuliwa kwake Bwana Yesu kutoka mbinguni pamoja na malaika wa uweza wake,


BASSI tunakusihini, ndugu, katika khabari ya kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo, na kukusanyika kwetu mbele yake,


Maana siku ya Bwana itakuja kama mwizi usiku; katika siku biyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na inchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.


Lakini Mikael, malaika mkuu, aliposhindana na Shetani, na kuhujiana nae kwa ajili ya mwili wa Musa, hakuthubutu kumshitaki kwa kumlaumu, bali alisema, Bwana akukemee.


Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana; nikasikia sauti kuu nyuma yangu, kama sauti ya baragumu,


Tazama yuaja na mawingu: na killa jicho litamwona, na hawo waliomchoma; na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amin.


Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Wa kheri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; na matendo yao yafuatana nao.


Nikaona, nikasikia tai akiruka kati kati ya mbingu, akisema kwa sauti kuu, Ole, ole, ole wao wakaao juu ya inchi, kwa sababu ya sauti zisaliazo za baragumu ya malaika watatu, walio tayari kupiga.


Nikawaona malaika saba wasimamao mbele za Mungu, wakapewa baragumu saba.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo