Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wathesalonike 4:14 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

14 Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu Mungu atawaleta pamoja nae.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Sisi tunaamini kwamba Yesu alikufa, akafufuka; na hivyo sisi tunaamini kwamba Mungu atawaleta pamoja na Yesu wale wote waliofariki wakiwa wanamwamini.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Sisi tunaamini kwamba Yesu alikufa, akafufuka; na hivyo sisi tunaamini kwamba Mungu atawaleta pamoja na Yesu wale wote waliofariki wakiwa wanamwamini.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Sisi tunaamini kwamba Yesu alikufa, akafufuka; na hivyo sisi tunaamini kwamba Mungu atawaleta pamoja na Yesu wale wote waliofariki wakiwa wanamwamini.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Tunaamini kwamba Isa alikufa na kufufuka. Na kwa hivyo, tunaamini kwamba Mungu atawaleta pamoja naye wale waliolala katika Isa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Kwa kuwa tunaamini kwamba Isa alikufa na kufufuka, na kwa hivyo, Mwenyezi Mungu kwa njia ya Isa atawafufua pamoja naye wale waliolala mautini ndani yake.

Tazama sura Nakili




1 Wathesalonike 4:14
16 Marejeleo ya Msalaba  

Nae atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya panda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka upande mmoja wa mwisho wa mbinguni mpaka upande wa pili.


Maana Kristo alikufa akafufuka akawa hayi tena kwa sababu hii, awamiliki waliokufa na walio hayi pia.


Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Yesu ataihuisha na miili yemi iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho yake anayekaa ndani yenu.


apate kuifanya imara mioyo yenu iwe bila lawama katika utakatifu mbele za Mungu, Baba yetu, wakati wa kuja kwake Bwaua wetu Yesu pamoja na watakatifu wake wote.


Lakini, ndugu, hatutaki msijue khabari zao waliolala, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini.


baada va haya sisi tulio hayi, tuliosalia, tutachukuliwa pamoja nao katika mawingu, illi tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.


BASSI tunakusihini, ndugu, katika khabari ya kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo, na kukusanyika kwetu mbele yake,


na aliye hayi; nami nalikuwa nimekufa, na tazama ni hayi hatta milele na milele. Amin. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.


Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Wa kheri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; na matendo yao yafuatana nao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo