Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wathesalonike 4:1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 ILIYOBAKI, ndugu, tunakusihini na kukuonyeni kuenenda katika Bwana Yesu, kama mlivyopokea kwetu, jinsi iwapasavyo kuenenda na kumpendeza Mungu, kama na muavyoenenda, mpate kuzidizidi sana.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Hatimaye, ndugu zangu, mmejifunza kutoka kwetu namna mnavyopaswa kuishi ili kumpendeza Mungu. Na kweli mmekuwa mnaishi hivyo. Sasa tunawaombeni na kuwasihi kwa jina la Bwana Yesu mfanye vema zaidi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Hatimaye, ndugu zangu, mmejifunza kutoka kwetu namna mnavyopaswa kuishi ili kumpendeza Mungu. Na kweli mmekuwa mnaishi hivyo. Sasa tunawaombeni na kuwasihi kwa jina la Bwana Yesu mfanye vema zaidi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Hatimaye, ndugu zangu, mmejifunza kutoka kwetu namna mnavyopaswa kuishi ili kumpendeza Mungu. Na kweli mmekuwa mnaishi hivyo. Sasa tunawaombeni na kuwasihi kwa jina la Bwana Yesu mfanye vema zaidi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Na kuhusu mambo mengine, ndugu, tuliwafundisha jinsi ya kuishi ili kumpendeza Mungu, kama vile mnavyoishi. Sasa tunawaomba na kuwasihi katika Bwana Isa mfanye hivi zaidi na zaidi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Hatimaye, ndugu, tuliwaomba na kuwasihi katika Bwana Isa kwamba, kama mlivyojifunza kutoka kwetu jinsi iwapasavyo kuishi ili kumpendeza Mwenyezi Mungu, kama vile mnavyoishi, imewapasa mzidi sana kufanya hivyo.

Tazama sura Nakili




1 Wathesalonike 4:1
44 Marejeleo ya Msalaba  

Kilia tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na killa lizaalo hulisafisha illi lizidi kuzaa.


Kwa maana sikujiepusha na kuwakhubirini khabari ya shauri lote la Mungu.


Wafuatao mambo ya mwili hawawezi kumpendeza Mungu.


Kwa maana mimi nalipokea kwa Bwana niliyowakhubirini, ya kuwa Bwana Yesu usiku ule aliotolewa alitwaa mkate,


NAWAARIFU, ndugu, injili niliyowakhubirieni; ndiyo mliyoipokea, katika hiyo mnasimama,


Bassi, ndugu wapendwa, mwe imara, msiotikisika, mkizidi sana kutenda kazi ya Bwana siku zote, kwa kuwa taabu yenu siyo burre katika Bwana.


NAMI Paolo, nawasihi kwa upole na utaratibu wa Kristo, mimi niliye mnyenyekevu niwapo pamoja nanyi, bali nisipokuwapo mwenye ujasiri kwenu;


Khatimae, ndugu, kwa kherini; mtimilike, mfarajike, nieni mamoja, mkae katika imani; na Mungu wa upendo na amani awe pamoja nanyi.


Kwa hiyo, tena, ikiwa tupo hapa, au ikiwa hatupo hapa, twajitahidi kumpendeza yeye.


NASI tukitenda kazi pamoja nae tunakusihini msiipokee neema ya Mungu burre,


NDUGU, mtu ajapogbafilika katika kosa lo lote, ninyi mlio wa Roho mrudini mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako nsijaribiwe wewe mwenyewe.


BASSI nawasihini, mimi niliye mfungwa katika Bwana, mwenende kama inavyoustahili wito wenu mlioitiwa,


Bali ninyi hamkujifunza hivi khabari za Kristo;


Kwa sababu hii msiwe wajinga, bali watu wanaofahamu nini mapenzi ya Bwana.


Lakini mwenendo wenu uwe kama inavyoipasa Injili ya Kristo, illi, nikija na kuwaona ninyi, au nisipokuwapo, niyasikie mambo yenu, kama mnasimama imara katika roho moja, kwa moyo mmoja mkiishindania imani ya Injili;


Na hii ndiyo sala yangu, pendo lenu lizidi kuwa jingi sana, katika hekima na ufahamu wote;


nakaza mwendo, niifikilie thawabu ya wito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu.


mwenende kama ilivyo wajib wenu kwa Bwana, mkimpendeza kabisa; kwa killa kazi njema mkizaa matunda, mkizidi katika maarifa ya Mungu;


Bassi kama mlivyompokea Kristo Yesu, Bwana, enendeni vivyo hivyo katika yeye,


Bwana na awaongozeni na kuwazidisheni katika upendo, ninyi kwa ninyi, na kwa watu wote, kama vile na sisi kwenu;


Maana mnajua maagizo gani tuliyowapeni kwa Bwana Yesu.


Lakini, ndugu, tunataka mwajue wale wanaojitaabisha kwa ajili yenu na kuwasimamieni katika Bwana, na kuwaonyeni;


Imetupasa kumshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu, ndugu, kama ilivyo wajib, kwa kuwa imani yenu inazidi sana, na upendo wa killa mtu kwenu kwa wenzake umekuwa mwingi.


BASSI tunakusihini, ndugu, katika khabari ya kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo, na kukusanyika kwetu mbele yake,


ILIYOBAKI, ndugu, tuombeeni, neno la Bwana liendelee, likatunzwe vilevile kama ilivyo kwenu;


Lakini, ninyi, ndugu, msikate tamaa katika kutenda mema.


Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Bwana Kristo Yesu, na mbele ya malaika wateule, yatende hayo pasipo kuhukumu kwa haraka; usifanye neno lo lote kwa upendeleo.


NAKUSHUHUDIA mbele za Mungu, na Bwana Yesu Kristo, atakaewahukumu walio hayi na waliokufa, kwa kudhihiri kwake, na kwa ufalme wake;


Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu ampendezae Mungu lazima aamini kwamba yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.


Lakini msisahau kutenda mema na kushirikiana na watu; maana sadaka kama hizi ndizo zimpendezazo Mungu.


Nawasihini, ndugu, livumilieni neno hili lenye maonyo; maana nimewaandikia kwa maneno machache.


Lakini, kaeni katika neema, na katika kumjua Bwana wetu, Mwokozi wetu, Yesu Kristo. Utukufu una yeye sasa na hatta milele. Amin.


na lo lote tuombalo, twalipokea kwake, kwa kuwa twazishika amri zake, na kuyatenda yapendezayo machoni pake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo