Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wathesalonike 3:6 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

6 Lakini Timotheo alipotujia siku hizi kutoka kwenu, akatuletea khabari njema za imani yenu na upendo wenu, na ya kwamba mnatukumbuka vema siku zote: mkitamani kutuona sisi vile vile kama sisi ninyi;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Sasa Timotheo amekwisha rudi, naye ametupa habari za kufurahisha kuhusu imani na upendo wenu. Ametuarifu kwamba mnatukumbuka daima, na kwamba mna hamu ya kutuona sisi kama nasi tulivyo na hamu ya kuwaoneni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Sasa Timotheo amekwisha rudi, naye ametupa habari za kufurahisha kuhusu imani na upendo wenu. Ametuarifu kwamba mnatukumbuka daima, na kwamba mna hamu ya kutuona sisi kama nasi tulivyo na hamu ya kuwaoneni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Sasa Timotheo amekwisha rudi, naye ametupa habari za kufurahisha kuhusu imani na upendo wenu. Ametuarifu kwamba mnatukumbuka daima, na kwamba mna hamu ya kutuona sisi kama nasi tulivyo na hamu ya kuwaoneni.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Lakini Timotheo amerejea kwetu hivi sasa kutoka kwenu, na ameleta habari njema kuhusu imani yenu na upendo wenu. Ametuambia kwamba siku zote mnatukumbuka kwa wema, na kwamba mna shauku ya kutuona kama vile sisi tulivyo na shauku ya kuwaona ninyi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Lakini sasa Timotheo ndiyo tu amerejea kwetu kutoka kwenu na ameleta habari njema kuhusu imani yenu na upendo wenu. Ametuambia kwamba siku zote mnatukumbuka kwa wema na kwamba mna shauku ya kutuona kama vile sisi tulivyo na shauku ya kuwaona ninyi.

Tazama sura Nakili




1 Wathesalonike 3:6
24 Marejeleo ya Msalaba  

AKAFIKA Derbe na Lustra, na hapo palikuwa na mwanafunzi mmoja jina lake Timotheo, mwana wa mwanamke mmoja Myahudi aliyeamini: lakini baba yake alikuwa Myunani.


BAADA ya mambo haya Paolo akatoka Athene akalika Korintho.


Hatta Sila na Timotheo walipotelemka kutoka Makedonia, Paolo akashurutishwa rohoni mwake, akiwashuhudia Wayahudi ya kwamba Yesu ni Kristo.


Tena nawasifu, ndugu, kwa sababu mmenikumbuka katika mambo yote, nanyi mmeyashika yale niliyowatolea vile vile kama nilivyowatolea.


Bassi, sasa inabaki imani, tumaini, upendo, hizi tatu; na iliyo kuu katika hizi ni upendo.


Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno wala kutokutahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo.


Maana Mungu ni shahidi wangu, jinsi ninavyowaonea shauku katika moyo wake Kristo Yesu.


tuliposikia khabari za imani yenu katika Kristo Yesu, na upendo mlio nao kwa watakatifu wote;


Salamu yangu mimi Paolo, kwa mkono wangu mwenyewe. Yakumbukeni mafungo yangu. Neema na iwe pamoja nanyi. Amin.


wala hatuachi kuikumbuka kazi yenu ya amani, na taabu yenu ya upendo, na uvumilivu wenu wa tumaini lililo katika Bwana Yesu Kristo, mbele za Mungu Baba yetu;


Lakini sisi, ndugu, tukifarakana nanyi kwa kitambo, kwa nso si kwa moyo, tulitamani zaidi kuwaona nyuso zenu, kwa shauku nyingi.


Maana, ndugu, mnakumbuka taabu yetu na masumbufu yetu; kwa kuwa mchana na usiku tulifanya kazi tusije tukamlemea mtu wa kwenu, tukawakhubirini bivi Injili ya Mungu.


kwa sababu hiyo tulifarijiwa, ndugu, kwa khabari zenu, katika shidda na mateso yetu yote, kwa imani yenu.


Imetupasa kumshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu, ndugu, kama ilivyo wajib, kwa kuwa imani yenu inazidi sana, na upendo wa killa mtu kwenu kwa wenzake umekuwa mwingi.


Bali kusudi la mausia hayo ni upendo utokao katika moyo safi na dhamiri njema, na imani isiyo na unafiki:


Namshukuru Mungu, nimwabuduye tangu zamani za wazee wangu kwa dhamiri safi, kama vile nikukumbukavyo wewe daima, katika kuomba kwangu, mchana na usiku, ninatamani sana kukuona,


nikisikia khabari ya upendo wako na ya imani uliyo nayo kwa Bwana Yesu na kwa watakatifu wote;


Wakumbukeni waliofungwa kana kwamba mmefungwa pamoja nao; nao wanaodhulumiwa, kwa kuwa nanyi m katika mwili.


Wakumbukeni wale waliokuwa na mamlaka juu yenu, waliowaambia neno la Mungu; tena, kwa kuuchunguza sana mwisho wa maisha zao, iigeni imani yao.


Na hii ndiyo amri yake, tuliamini jina la Mwana wake Yesu Kristo, na kupendana, kama alivyotupa amri.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo