Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wathesalonike 3:2 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

2 tukamtuma Timotheo ndugu yetu, mtumishi wa Mungu, mfanya kazi pamoja naswi katika Injili ya Kristo, kuwafanya ninyi imara na kuwafariji kwa ajili ya imani yenu,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 na kumtuma kwenu ndugu yetu Timotheo, ambaye ni mfanyakazi mwenzetu kwa ajili ya Mungu katika kuhubiri Habari Njema ya Kristo. Tulimtuma ili awaimarisheni na kuwafarijini,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 na kumtuma kwenu ndugu yetu Timotheo, ambaye ni mfanyakazi mwenzetu kwa ajili ya Mungu katika kuhubiri Habari Njema ya Kristo. Tulimtuma ili awaimarisheni na kuwafarijini,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 na kumtuma kwenu ndugu yetu Timotheo, ambaye ni mfanyakazi mwenzetu kwa ajili ya Mungu katika kuhubiri Habari Njema ya Kristo. Tulimtuma ili awaimarisheni na kuwafarijini,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Tukamtuma Timotheo ambaye ni ndugu yetu na mtumishi mwenzetu wa Mungu katika kuieneza Injili ya Al-Masihi, aje kuwaimarisha na kuwatia moyo katika imani yenu,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Tukamtuma Timotheo ambaye ni ndugu yetu na mtumishi mwenzetu wa Mungu katika kuieneza Injili ya Al-Masihi, aje kuwaimarisha na kuwatia moyo katika imani yenu,

Tazama sura Nakili




1 Wathesalonike 3:2
24 Marejeleo ya Msalaba  

AKAFIKA Derbe na Lustra, na hapo palikuwa na mwanafunzi mmoja jina lake Timotheo, mwana wa mwanamke mmoja Myahudi aliyeamini: lakini baba yake alikuwa Myunani.


Makanisa yakatiwa nguvu kwa imani, hesabu yao ikaongezeka killa siku.


Hatta Sila na Timotheo walipotelemka kutoka Makedonia, Paolo akashurutishwa rohoni mwake, akiwashuhudia Wayahudi ya kwamba Yesu ni Kristo.


Timotheo, mtenda kazi pamoja nami, awasalimu, na Lukio, na Yason, na Sosipatro, jamaa zangu.


Kwa kadiri ya neema ya Mungu niliyopewa, mimi, kama mkuu wa wajenzi mwenye hekima, nimeuweka msingi, na mtu mwingine anajenga juu yake. Lakini killa mtu na aangalie jinsi anavyojenga juu yake.


Kwa hiyo nalimtuma Timotheo kwenu, aliye mwana wangu mpendwa, mwaminifu katika Bwana, atakaewakumbusha njia zangu zilizo katika Kristo, kama nifundishavyo killa pahali katika killa kanisa.


PAOLO, mtume wa Yesu Kristo kwa mapenzi ya Mungu, na Timothieo ndugu yetu, kwa kanisa la Mungu lililo katika Korintho, pamoja na watakatifu wote walio katika inchi yote ya Akaia:


Maana Mwana wa Mungu, Yesu Kristo, aliyekhubiriwa na sisi kati yenu, na mimi na Silwano na Timotheo, hakuwa ndiyo na siyo; bali katika yeye ndiyo imepata kuwako.


Bassi nilipofika Troa kwa ajili ya Injili ya Kristo nikafunguliwa mlango katika Bwana,


sikupata raha nafsini mwangu, kwa sababu sikumwona Tito ndugu yangu, bali niliagana nao, nikaondoka kwenda Makedonia.


Bassi mtu akitaka khabari za Tito, yeye ni mshirika wangu, na mtenda kazi pamoja nami; tena akitaka khabari za ndugu zetu, wao ni mitume ya makanisa, na utukufu wa Kristo.


Nami nikitumaini haya, najua ya kuwa nitakaa na kudumu pamoja nanyi, illi muendelee mkapate kufurahi katika imani;


PAOLO, mtume wa Yesu Kristo kwa mapenzi ya Mungu, na Timotheo ndugu yetu,


kama mlivyofundishwa na Epafra mjoli wetu mpenzi, aliye mkhudumu amini wa Kristo kwa ajili yenu;


Epafra, aliye mtu wa kwenu, mtumwa wa Yesu Kristo, awasalimu, akifanya bidii siku zote kwa ajili yenu, katika maombi yake msimame wakamilifu mkathuhutike sana katika mapenzi yote ya Mungu.


pamoja ua Onesimo, ndugu mwaminifu, mpendwa, aliye mtu wa kwenu; watawaarifuni mambo yote ya huku.


apate kuifanya imara mioyo yenu iwe bila lawama katika utakatifu mbele za Mungu, Baba yetu, wakati wa kuja kwake Bwaua wetu Yesu pamoja na watakatifu wake wote.


Kwa hiyo mimi nami nilipokuwa siwezi kuvumilia tena, nalimtuma mtu illi niijue imani yenu, asije yule mjaribu akawajaribu, wala taabu yetu isiwe haina faida.


awafariji mioyo yenu, na kuwafanya imara katika killa neno na tendo jema.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo