Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wathesalonike 3:13 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

13 apate kuifanya imara mioyo yenu iwe bila lawama katika utakatifu mbele za Mungu, Baba yetu, wakati wa kuja kwake Bwaua wetu Yesu pamoja na watakatifu wake wote.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Hivyo ataiimarisha mioyo yenu, nanyi mtakuwa wakamilifu na watakatifu mbele ya Mungu na Baba yetu wakati Bwana wetu Yesu atakapokuja pamoja na wote walio wake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Hivyo ataiimarisha mioyo yenu, nanyi mtakuwa wakamilifu na watakatifu mbele ya Mungu na Baba yetu wakati Bwana wetu Yesu atakapokuja pamoja na wote walio wake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Hivyo ataiimarisha mioyo yenu, nanyi mtakuwa wakamilifu na watakatifu mbele ya Mungu na Baba yetu wakati Bwana wetu Yesu atakapokuja pamoja na wote walio wake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Tunamwomba Mungu aimarishe mioyo yenu ili msiwe na lawama katika utakatifu mbele za Mungu wetu aliye Baba yetu wakati wa kuja kwake Bwana wetu Isa pamoja na watakatifu wote.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Tunamwomba Mwenyezi Mungu aimarishe mioyo yenu ili msiwe na lawama katika utakatifu mbele za Mungu wetu aliye Baba yetu wakati wa kuja kwake Bwana Isa pamoja na watakatifu wote.

Tazama sura Nakili




1 Wathesalonike 3:13
28 Marejeleo ya Msalaba  

Hatta atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja nae, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake:


Maana killa mtu atakaenionea haya mimi, na maneno yangu, katika kizazi hiki cha zina na dhambi, Mwana wa Adamu atamwonea haya yeye atakapokuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu.


Nao wote wawili wenye haki mbele ya Mungu, wakiendelea katika amri zote za Bwana na hukumu zake zote bila lawama.


Wewe u nani unaemhukumu mtumishi wa mwingine? Kwa Bwana wake mwenyewe husimama au huanguka. Naam, atasimamishwa, maana Bwana aweza kumsimamisha.


Sasa na atukuzwe yeye awezae kutufanya imara kwa injili yangu na kwa kukhubiriwa Yesu Kristo, kwa ufunuo wa ile siri iliyostirika tangu zamani za milele,


Lakini killa mmoja mahali pake; limbuko Kristo; baadae walio wake Kristo, atakapokuja.


aliyejitoa nafsi yake kwa ajili ya dhambi zetu illi atuokoe na dunia hii mbovu iliyopo sasa, kama alivyopenda Mungu, Baba yetu:


apate kujiletea Kanisa tukufu lisilo na ila ama kunyanzi ama lo lole kama haya; bali liwe takatifu na lisilo na mawaa.


mpate kuyakubali yaliyo mema; illi mwe na mioyo safi, bila kosa, mpaka siku ya Kristo,


katika mwili wa nyama yake, kwa kufa kwake, illi awalete ninyi mbele zake, watakatifu, hamna mawaa wala lawama,


Maana tumnini letu, au furaha yetu, an taji ya kujisifu ni nini? Si ninyi, mbele za Bwana wetu Yesu Kristo wakati wa kuja kwake?


Bassi Mungu mwenyewe, Baba yetu, na Bwana wetu Yesu Kristo atuongoze njia yetu tufike kwenu;


tukamtuma Timotheo ndugu yetu, mtumishi wa Mungu, mfanya kazi pamoja naswi katika Injili ya Kristo, kuwafanya ninyi imara na kuwafariji kwa ajili ya imani yenu,


Maana twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hayi, tutakaosalia hatta wakati wa kuja kwake Bwana, hatutawatangulia wao waliokwisha kulala.


baada va haya sisi tulio hayi, tuliosalia, tutachukuliwa pamoja nao katika mawingu, illi tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.


Mungu wa amani mwenyewe awatakase kahisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.


atakapokuja illi kutukuzwa katika watakatifu wake, na kuajabiwa katika wote waaminio (kwa sababu ushuhuda wetu ulisadikiwa kwenu), katika siku ile.


na kuwalipa ninyi mteswao raha pamoja na sisi wakati wa kufunuliwa kwake Bwana Yesu kutoka mbinguni pamoja na malaika wa uweza wake,


BASSI tunakusihini, ndugu, katika khabari ya kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo, na kukusanyika kwetu mbele yake,


Bassi, na ninyi subirini, jithubutisheni mioyo yenu, kwa maana kuja kwake Bwana kunakaribia.


Na Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia utukufu wake wa milele katika Kristo, mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, yeye mwenyewe atawatengeneza, atawathubutisha, atawatia nguvu.


Na Enok, wa saba baada ya Adamu, alitoa maneno ya unabii juu ya hawo, akisema, Angalia, Bwana alikuja na elfu kumi za watakatifu wake,


Kwake Yeye awezae kuwalinda ninyi msijikwae, na kuwasimamisha mbele ya utukufu wake bila mawaa katika furaha kuu,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo