Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




1 Wathesalonike 3:10 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

10 usiku na mchana tukiomba kwa juhudi tupate kuwaona nyuso zenu na kuyatengeneza mapungufu ya imani yenu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Tunazidi kumwomba Mungu usiku na mchana kwa moyo wetu wote ili atupatie fursa ya kuwaoneni uso kwa uso ili tuweze kurekebisha chochote kilichopungua katika imani yenu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Tunazidi kumwomba Mungu usiku na mchana kwa moyo wetu wote ili atupatie fursa ya kuwaoneni uso kwa uso ili tuweze kurekebisha chochote kilichopungua katika imani yenu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Tunazidi kumwomba Mungu usiku na mchana kwa moyo wetu wote ili atupatie fursa ya kuwaoneni uso kwa uso ili tuweze kurekebisha chochote kilichopungua katika imani yenu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Usiku na mchana tunaomba kwa bidii ili tupate kuwaona tena na kujaza kile kilichopungua katika imani yenu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 Usiku na mchana tunaomba kwa bidii ili tupate kuwaona tena na kujaza kile kilichopungua katika imani yenu.

Tazama sura Nakili




1 Wathesalonike 3:10
19 Marejeleo ya Msalaba  

nae mjane wa miaka themanini na mine; asiyeondoka hekaluni, kwa kufunga na kusali akiabudu usiku na mchana.


ambayo kabila zetu thenashara wanataraja kuifikia, wakimkhudumu Mungu kwa bidii mchana na usiku. Nami ninashitakiwa na Wayahudi kwa ajili ya tumaini hilo, ee Mfalme.


Na nikiwa na timiaini hilo nalitaka kwenda kwenu hapo kwanza, illi mpate karama ya pili;


Si kwamba tunatawala imani yenu; hali tu wasaidizi wa furaha yenu; maana mnasimama kwa imani.


Khatimae, ndugu, kwa kherini; mtimilike, mfarajike, nieni mamoja, mkae katika imani; na Mungu wa upendo na amani awe pamoja nanyi.


Maana twafurahi, sisi tulipo dhaifu, na ninyi hodari. Tena twaomba hili nalo, mtimilike.


Nami nikitumaini haya, najua ya kuwa nitakaa na kudumu pamoja nanyi, illi muendelee mkapate kufurahi katika imani;


ambae sisi tunakhubiri khabari zake, tukimwonya killa mtu, na tukimfundisha killa mtu katika hekima yote, tupate kumleta killa mtu mtimilifu katika Kristo Yesu;


Epafra, aliye mtu wa kwenu, mtumwa wa Yesu Kristo, awasalimu, akifanya bidii siku zote kwa ajili yenu, katika maombi yake msimame wakamilifu mkathuhutike sana katika mapenzi yote ya Mungu.


Bassi Mungu mwenyewe, Baba yetu, na Bwana wetu Yesu Kristo atuongoze njia yetu tufike kwenu;


Kwa hiyo twawaombea ninyi siku zote, illi Mungu wetu awahesabu kuwa nimeustahili wito wenu, akatimize killa haja ya wema na killa kazi ya imani kwa nguvu:


Namshukuru Mungu, nimwabuduye tangu zamani za wazee wangu kwa dhamiri safi, kama vile nikukumbukavyo wewe daima, katika kuomba kwangu, mchana na usiku, ninatamani sana kukuona,


Na pamoja na hayo uniwekee tayari mahali pa kukaa: maana nataraja ya kwamba kwa maombi yenu mtajaliwa kunipata.


Na hawa nyama wane, wenye uhayi, killa mmoja alikuwa na mabawa sita: pande zote na ndani wamejaa macho, nao hawapumziki mchana wala usiku, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Bwana Mungu Mwenyiezi, aliyekuwako, nae yuko, nae anakuja.


Kwa hiyo wako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, nao wanamtumikia mchana na usiku katika hekalu lake, na yeye aketiye katika kiti cha enzi atatanda khema yake juu yao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo